Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tutatoa ruzuku hadi bei mafuta ikae sawa duniani-Samia
Habari za SiasaTangulizi

Tutatoa ruzuku hadi bei mafuta ikae sawa duniani-Samia

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kukata matumizi yake kila mwezi na kutoa ruzuku ya mafuta hadi pale bei itakapokuwa sawa katika soko la dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Serikali ilianza kutoka zuruku ya Sh 100 bilioni mwezi huu na kuleta ahueni kwenye bei za nishati ya mafuta ambapo Petroli ilipungua kwa Sh 152 hadi 306 na dizeli Sh 320 hadi 488 kutegemeana na eneo.

Ruzuku hiyo iliyoanza kutumika tarehe 1 Juni, 2022, ilipunguza bei za mafuta ya petroli kutoka Sh 3,301 hadi 2,994 na dizeli kutoka 3,452 hadi 3,131 kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza na wananchi wa Bwanga mkoani Geita akielekea mkoani Kagera, leo Jumatano tarehe 8 Juni, 2022, Rais Samia amesema, “tunajaribu kutoa ruzuku kama mlisikia mwezi uliopita nilisema nitatoa Sh 100 bilioni ili bei zishuke na mwezi huu bei zimeshuka tutaendelea kutoa hiyo ruzuku hadi dunia ikae sawa tutaendelea kukata matumizi ya Serikali kutoa ruzuku mpaka bei zikae sawa.”

Amesema jitihada zingine Serikali inayofanya ni kuziambia nchi zinazopigana (Urusi na Ukreani) kuacha mapigano ili mambo yawe sawa.

“Tunachokifanya ili kupunguza makali dunia nzima tunaziambia zile nchi mbili ziache kupigana kwasababu zikiacha kupigana tunapata manufaa mengi tu,” amesema Rais Samia.

Akifafanua kwa wananchi namna vita hiyo inavyoathiri upandaji wa bei za bidhaa Rais Samia amesema moja ya nchi iliyokuwa inategemewa kwa gesi katika Mataifa ya Magharibi ipo vitani na hivyo kusababisha nchi hizo kugeukia mafuta.

Ameeleza zaidi kuwa hali hiyo imesababisha kuwepo mahitaji makubw aya mafuta na kusababisha bei kupanda kwa kasi.

Mkuu huyo wa nchi ameendelea kueleza kuwa bei kubwa ya mafuta imesababisha kuongezeka kwa gharama ya kusafirisha bidhaa ambapo amesema kontena lilikuwa likisafirishwa kwa dola 1,800 hivi sasa linasafirshwa kwa dola 8,000 hadi 9,000.

“Lakini mafuta yanavyopanda yakifika hapa kwetu mwenye gari ananunua kwa bei kubwa kwahiyo na yeye anarudisha kwenye nauli hata bodaboda mmenunua mafuta na mmepandisha bei,” amesema.

1 Comment

  • Serikali kukata matumizi? Kweli? Naomba kujua ni wapi wamekata matumizi. Ebu tusaidiane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!