Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Tulisalitiwa, tunapambana wenyewe – CUF
Habari za Siasa

Tulisalitiwa, tunapambana wenyewe – CUF

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeeleza dhamira yake ya kuking’oa Chama Cha Mapinduzi (CCM), bila kushirikiana na chama chochote. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kimeeleza, tayari kina donda la muda mrefu la usaliti kutokana na ushirikiano wake na vyma vingine vya upinzani (Ukawa), na sasa kuendesha siasa za kukikabili chama tawala kwenye chaguzi zijazo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizo leo tarehe 23 Oktoba 2019, Jafari Mneke, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF amesema, usaliti unawaweka pembeni na ushiriki katika vyama vingine vya siasa.

“Tunaingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa bila kushirikiana na chama chochote bila kushirikiana na chama chochote kile, kwa sababu hatujaona chama chenye dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM. Kwa muda huu tunaingia kama CUF kuiondoa CCM madarakani,” amesema Mneke.

Amesema, hatua ya baadhi ya wafuasi wa CUF kuhamia Chama cha ACT-Wazalendo ni muendelezo wa propaganda za kisiasa, kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa waliohama ni wanachama wa chama chake.

“Suala la mwanachama kuhama chama cha siasa ni suala la demokrasia pia ni haki ya kikatiba, lakini pamoja na uhalisia huo, ulichosema Zitto jana hakina uhalisia, ni propaganda zilizozungumzwa. Hakuna ushahidi wa kwamba waliohama ni wanachama au viongozi wa CUF,” amesema Mneke na kuongeza;

“Ni propaganda zimefanywa maeneo mbalimbali, wanasema kuna maelfu ya wanachama wamehamia ACT, lakini ukienda kutazama hakuna watu kama hao. Ni watu miongoni mwao wamejibadilisha majina wakajiita viongozi ama wanachama wa CUF.”

Mneke amesema, CUF hatishwi na ACT-Wazalendo, akieleza kwamba chama hicho (CUF) ni chuma cha pua.

“Ni msamiati mwepesi, wanajitekenya wenyenyewe na wanacheka wenyewe, sisi hatutishwi na ACT Wazalendo, CUF ni imara, itabaki kuwa imara. Imepita katika tanuru la moto, imekuwa ni chuma cha pua. Yaani ni imara kuliko zamani,” amesema Mneke.

Akizungumza kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Mnene amesema chama hiko kiko katika mchakato wa kuteua wajumbe watakaoshiriki kwenye uchaguzi huo.

“Mpaka kufika tarehe 26 mwezi huu, itakuwa tayari tushakamilisha mchakato wa kupata wagombea,” amesema Mneke.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!