Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CUF wapata pigo, Maalim Seif, Prof. Lipumba waungana
Habari za SiasaTangulizi

CUF wapata pigo, Maalim Seif, Prof. Lipumba waungana

Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimepata pigo kwa kuondokewa na Muasisi wake, Mzee James Mapalala, aliyefariki dunia leo tarehe 23 Oktoba 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mzee Mapalala amefariki dunia katika Hospitali ya Kairuki, jijini Dar es Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, ameungana na Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa chama hicho taifa, kuomboleza kifo cha Mzee Mapalala.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Maalim Seif amesema amepokea kwa masikitiko kifo cha muasisi huyo wa CUF.

Maalim Seif amesema, Mzee Mapalala atakumbukwa kwa mchango wake alioutoa enzi za uhai wake, katika kupigania mageuzi ya kisiasa hapa nchini.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mzee James Kabalo Mapalala, aliyekuwa Mwenyekiti wa mwanzo wa CUF, kilichotokea leo Hospitali ya Kairuki, jijini Dar es Salaam. Mzee Mapalala atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kupigania mageuzi ya kisiasa hapa nchini,”  ameandika Maalim Seif.

Wakati huo huo, Prof. Lipumba amesema CUF imepata pigo kwa kuondokewa na Mzee Mapalala, na kueleza kwamba, chama hicho kitaukumbuka mchango wake, hasa katika kuimarisha demokrasia.

Prof. Lipumba amesema, kwa kuthamini mchango wa Mzee Mapalala, CUF itasimamisha bendera zake nusu mringoti nchi nzima, hadi pale mwilo wake utakapozikwa.

“Tumepata taarifa za msiba, taratibu za mazishi hatujapata kwa ukamilifu lakini tutashiriki mazishi yake kwa kuuthamini mchango wake. Natoa agizo nchi nzima kuweka bendera nusu mringoti mpaka siku ya mazishi. Hii ni kuuenzi mchango wake,” amesema Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba amesema Mzee Mapalala ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho, ambaye alikijenga enzi za uhai wake. Na kufanikiwa kuweka mizizi ya chama hicho Visiwani Zanzibar na Tanzania Bara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!