Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tuiambie dunia inatosha – Prof. Kabudi
Habari za Siasa

Tuiambie dunia inatosha – Prof. Kabudi

Prof. Palamagamba Kabudi
Spread the love

PROFESA Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, amewataka wananchi kutotikiswa na vitisho vya kunyimwa misaada ya fedheha kutoka mataifa ya nje. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Prof. Kabudi ametoa wito huo leo tarehe 25 Oktoba 2019, katika kongamano maalumu la ‘ Vikwazo vya Kiuchumi na Hatma ya Maendeleo ya Afrika’ iliyofanyika Huo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema, vijana wengi wakiona nchi inatishiwa kunyimwa misaada, wanahangaika “tukitishiwa kidogo, vijana wanahangaika. Tutakosa misaada, misaada ya fedheha. Ni mwanzo wa hatua ya kuiambia dunia enough is enough (inatosha inatosha),” amesema Prof. Kabudi.

Waziri Kabudi ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia hatua ya Jumuiya za Kimataifa, kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbabwe.

Akizungumzia vikwazo hivyo, Prof. Kabudi amesema ni msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba vikwazo vilivyopo dhidi ya nchi ya Zimbabwe ni kinyume cha sheria.

“Kwa msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vikwazo hivi ni kinyume na sheria,” amesema Prof. Kabudi na kwamba Tanzania inazitaka Jumuiya za Kimataifa, kuiondolea Zimbabwe vikwazo hivyo.

“Leo ni siku ya kuiambia dunia, ondoeni vikwazo dhidi ya Zimbabwe, hatusemi Zimbabwe ni nchi iliyokamilika. Hatua zimechukuliwa kuondoa mapungufu yaliyokuwepo, leo sio siku ya kuomba, ni siku ya kutamka,” amesema Prof. Kabudi.

Amezitaka jumuiya na nchi zenye malalamiko dhidi ya Zimbabwe hasa Marekani na Umoja wa Ulaya (EU), kupeleka hoja zao za msingi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), ili zifanyiwe kazi na kisha kutoa maazimio kuhusu hoja zao.

“Marekani na Umoja wa Ulaya kama wana hoja ya msingi, wapeleke maazimio kwa Baraza la Amani la Umoja wa Taifa, na azimio litakalotoka, litakuwa ni azimio litakaloheshimika,” amesema Prof. Kabudi.

Waziri huyo wa Mambo wa Nje wa Tanzania, amesema kuiwekea vikwazo Zimbabwe ni sawa na kuzishambulia nchi za Afrika.

Pia, amesema vikwazo hivyo ni kinyume cha sheria na uvunjifu wa haki za binadamu, kwani wanaoathirika ni wanawake, watoto na wazee kwa kukosa huduma za kijamii.

“Aina hii ya vikwazo vimepitiliza, na sio tu vinakwenda kinyume na desturi, vinavunja haki za msingi za binadamu. Waathirika wakubwa ni wanawake, watoto na wazee.

“…ndio maana Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika maazimio yake ya mwaka 2014, limelaani aina hii ya vikwazo ambavyo vinatumika kama nyenzo ya kisiasa, kuweka vizuizi vya kiuchumi kwa nchi nyingine,” amesema Prof. Kabudi na kuongeza;

“Azimio hilo limerudiwa na Umoja wa Mataifa la tarehe 17 Desemba 2017, kueleza kwamba aina hii ya vikwazo si sahihi na si muafaka katika kutatua matatizo.”

Akitoa mada kuhusu nafasi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Prof. Godius Kahyarara, Profesa Mshiriki wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, jumuiya hiyo itaendelea kushinikiza jumuiya za kimataifa kuondoa vikwazo hivyo.

Prof. Kahyarara amesema, SADC ina nafasi kubwa katika kuhakikisha kwamba Zimbabwe inaondolewa vikwazo hivyo.

“Vikwazo vya kiuchumi tusichukulie ni vikwazo tu, yale ni mashambulio, wanapararaizi uchumi, haki za binadamu huduma za afya.

“Vikwazo vya kiuchumi vina madhara makubwa, vinaathiri uchumi na vinavuruga siasa. Vinapaswa kuondolewa mara moja,” amesema Prof. Kahyarara.

Wang Ke, Balozi wa China nchini Tanzania amesema, serikali yake inaungana na Tanzania kupinga vikwazo hivyo, kwa kuwa vinapingana na Sheria za Kimataifa.

“Tunaiunga mkono Tanzania kutaka Zimbabwe viondolewe, vinakwenda kinyume na sheria za kimataifa. Nachukua nafasi hii kwa niaba ya Serikali ya China kuonesha mshikamano wetu, na tutazungumza na jumuiya zingine kuhakikisha Zimbabwe inaondolewa vikwazo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!