July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM yaikingia kifua Zimbabwe

Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeeleza kutofurahishwa na hatua ya Zimbabwe kuwekewa vikwazo tangu mwaka 2000. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba 2019, Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) amesema, “inatosha.”

Amesema, kwa muda mrefu taifa hilo limekuwa likionewa na kufanyiwa vitendo vya unyanyaswaji, na kwamba Zimbabwe inahitaji kukua kiuchumi, kijamii na kibiashara.

Hivi karibuni Zimbabwe imeongezewa vikwazo baada ya askari wake kutuhumiwa kutumia silaha za moto dhidi ya waaandamanaji, waliokuwa wakipinga Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuchelewa kutangazwa matokeo ya urais.

Kwenye uchaguzi huo, Rais Emmerson Mnangagwa alitangazwa kuwa mshindi wa urais.

Mangula amesema, Rais John Magufuli analaani vikwazo dhidi ya Zimbabwe, na kutaka kuondolewa bila masharti yoyote.

“Kwa tamko hili tunaweka msisitizo na kupitia kwa Serikali za Tanzania, SADC na Afrika Mashariki (EAC) kwamba ifike wakati Umoja wa Afrika uchukue nafasi yake na kusimamia haki za wanachama ambao wanaendelea kuonewa kwa nguvu za kibeberu na ukoloni mamboleo,” amesema Mangula.

Marekani imemwekea vikwazo balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Anselem Sanyatwe kwa tuhuma za kuamuru wanajeshi wa nchi hiyo, kuwafyatulia risasi za moto waandamanaji hao.

error: Content is protected !!