Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwanachuo UDSM achafua hewa mbele ya waziri mkutanoni
Habari za SiasaTangulizi

Mwanachuo UDSM achafua hewa mbele ya waziri mkutanoni

Spread the love

MWOJA Aloyce, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amechafua hali ya hewa katika Kongamano Maalum la ‘Vikwazo vya Kiuchumi na Hatma ya Maendeleo ya Afrika’. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akichangia hoja, Mwoja alizua gumzo, baada ya kuhoji kutokuwepo kwa washiriki wa vyama vya siasa vya upinzani, katika kongamano hilo.

Mbele ya Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na viongozi wengine, wanachuo huyo alionesha kushangazwa na ‘ubaguzi’, akisema amewaona wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakishiriki kongamano hilo pasipo wawakilishi kutoka vyama vya upinzani.

“Naona wawakilishi kwenye kongamano hili kutoka CCM lakini sioni kutoka upinzani, kwanini?” amehoji mwanachuo huyo huku akisisitiza “inaonesha umoja haukuzingatiwa.”

Akikwepa kujibu hoja ya Mwoja, Dk. Godfrey Sansa, Mhadhiri Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alijielekeza katika kushauri masuala ya siasa kutoingizwa katika vyuo vikuu.

Akisisitiza kile alichoeleza, Dk. Sansa amewataka wanafunzi kutounda makundi ya kisiasa vyuoni.

“Tusiruhusu masuala ya kisiasa yakaingia kwa wasomi wetu. Viongozi tuwafundishe, vyuo vyetu viwe huru kwa itikadi. Lakini tuwafundishe uongozi ili atakapo maliza, awe kiongozi bora,” amesema Dk. Sansa na kuongeza;

“Tuache kufanya makundi ya vyama kwenye vyuo vikuu, katika hilo huwa sipepesi macho, atakayechukia achukie. Sasa hivi kuna mgawanyo hawa wa chama fulani, sisi sote ni wanafunzi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!