Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TRA yataja viwango vipya kodi ya majengo inayotozwa kupitia luku
Habari Mchanganyiko

TRA yataja viwango vipya kodi ya majengo inayotozwa kupitia luku

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetangaza viwango vipya vya kodi ya majengo vinavyokusanywa kwa kutumia njia ya ununuzi wa umeme kwa wamiliki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 4 Mei 2023 na TRA, viwango vya utozaji kodi ya majengo kwa mujibu wa mabadiliko ya kifungu cha 6 Cha Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali ya Mitaa (ukadiriaji), yaliyofanyika kupitia Sheria ya Fedha Na. 3 ya 2021.

Viwango hivyo vipya ni pamoja na, kiasi cha Sh. 12,000 kwa mwaka kwa nyumba ya kawaida. Sh. 60,000 kwa mwaka kwa kila sakafu ya  nyumba ya ghorofa katika maeneo ya majiji, manispaa na halmashauri.

Nyumba ya ghorofa katika maeneo ya halmashauri za wilaya, itatozwa kiasi cha Sh. 60,000 Kila mwaka.

Awali, kiwango cha kodi hiyo ilikuwa Sh. 12,000 kwa majengo yote.

Taarifa ya TRA imesema kuwa, kwa sasa uhakiki wa majengo ya ghorofa unaendelea kufanyika na Miata husika kuwekewa kiwango stahiki kulingana na aina ha jengo.

TRA inakusanya kodi hizo kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!