Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko ACT Wazalendo yaitaka jamii kulinda watoto
Habari Mchanganyiko

ACT Wazalendo yaitaka jamii kulinda watoto

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetoa wito kwa jamii kuhakikisha watoto wanalindwa ili kufikia malengo yao ikiwamo kutimiza ndoto ya kuwa viongozi imara kwa maslahi ya Taifa. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 4 Mei 2023 na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania-Bara, Dorothy Semu alipotembelea kituo cha kulea watoto yatima cha Sara House kilichopo Mwandege wilayani Mkurunga ,Mkoa wa Pwani.

Dorothy akiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa chama hicho pamoja na Naibu Katibu wa Uenezi,  Janeth Rithe; Katibu wa Ngome ya wanawake, Bonifacia Mapunda; Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Sevilina Mwijage  na Mwenyeji wao Katibu wa ACT-Pwani,Mohammed Mtambo na wanachama wengine waandamizi wa chama hicho.

Dorothy amesema kuwalinda watoto ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanakuwa salama kisaikolojia na kimwili ili kupata viongozi imara watakaoliongoza taifa .

“Suala la ulinzi wa watoto ni wajibu wetu sote, kila mtu ahusike katika kumlinda mtoto wa Kitanzania ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama na kuepushwa madhara ya kisaikolojia au kimwili”,  Dorothy.

Amesema ripoti za haki za binadamu ya mwaka 2022, ilionyesha kuwa matendo ya unyayasaji kwa watoto yameongezeka na kwamba hali hiyo haina ustawi mzuri wa watoto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!