Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaahidi kuhakikisha tasnia ya habari inasonga mbele
Habari Mchanganyiko

Serikali yaahidi kuhakikisha tasnia ya habari inasonga mbele

Spread the love

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amesema Serikali imeahidi kuhakikisha tasnia ya habari inasonga mbele kwa kutatua changamoto na kutekeleza masuala mbalimbali yanayoihusu tasnia hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kundo ameyasema hayo leo Zanzibar wakati wa Maadhimisho ya miaka 30 ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika tarehe 3 Mei ya kila mwaka .

 

“Ili kuhakikisha tasnia ya habari inasonga mbele, Serikali inaendelea kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kupeleka marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari Na.12 ya Mwaka 2016, vile vile tumeendelea na mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango ili kuona namna bora ya kushughulikia suala la kuondoa ushuru, forodha na kodi ya ongezeko la thamani kwenye karatasi na wino”, alisema Mhandisi Kundo.

Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kukuza teknolojia ya kijiditali ili kuharakisha maendeleo na kuendelea kusimamia Wanahabari katika kujitathmini na kujadiliana kwa uwazi ili kuruhusu mazingira ya kazi zao kuwa rafiki.

Aidha, Kundo amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar kwa kazi kubwa ambayo wameifanya kwenye tasnia ya habari ambapo ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wao hakuna chombo cha habari kilichofungiwa. Vile vile amewashukuru kwa uongozi wao ambao umewapa maono ya kuifanya Tanzania kuwa na uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.

Kwa upande mwingine, Kundo amewashukuru UNESCO kwani kwa miaka 32 mfululizo wameendelea kuwa wafadhili wa maadhimisho haya na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi pamoja nao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!