MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), inatarajia kutoa tuzo kwa waandishi wa habari bora wa taarifa za hali ya hewa pamoja na taa
rifa za mamlaka hiyo kwa ujumla kwa lengo la kutambua mchango wao katika sayansi ya hali ya hewa nchini. Anaripoti Rhoda Kanuti, Dar es salaam… (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma leo tarehe 14 Aprili 2022 na TMA kupitia Kitengo cha Masoko na Mahusiano, mamlaka hiyo imeandaa tuzo na zawadi hizo kutoa hamasa na kutambua mchango wa waandishi wa habari katika Sayansi ya Hali ya Hewa nchini.
“Tumeandaa utaratibu wa kutoa tuzo au zawadi maalum kwa waandishi wa habari bora kwa taarifa za hali ya hewa na TMA kwa ujumla” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa waandishi hao, watapatikana kwa uchambuzi wa kina utakaofanywa na kamati maalum itakayoundwa kupitia habari zote zitakazowasilishwa.
Waandishi wa habari wanatakiwa, kuwasilisha habari zao kupitia njia ya barua pepe ya media @meteo.go.tz.
Pia imesema kazi zitakazoshindanishwa ni zile zilizoripotiwa kuanzia mwenzi Oktoba mwaka 2021 mpaka mwezi Mei 2022.
Leave a comment