MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umewapa mafunzo ya namna kufuatilia na kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, wadau kutoka Asasi za Kiraia (AZAKI), za Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).
Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Jumanne, tarehe 15 Machi 2022, katika Hoteli ya Golden Tulip, visiwani Zanzibar na kufunguliwa na Meya wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Musa.
Akifungua mafunzo hayo, Mussa amewataka washiriki hao zaidi ya 50, kuyatumia katika kutokomeza changamoto za ukatili wa kijinsia visiwani humo.
“Nawasihi muwe mabalozi wazuri kuhakikisha kwamba udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto, kuhakikisha tatizo hili linaondoka katika nchi yetu,”amesema Mussa.
Kwa upande wake Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo juu ya namna ya kufuatilia, kuhifadhi na kutoa taarifa zinazogusa masuala ya udhalilishaji wa kijinsia hususan wanawake na watoto.
“Tunafahamu Zanzibar ina changamoto mbalimbali za haki za binadamu, hasa zinazogusa masuala ua udhalilishaji, mfano dawa za kulevya na mambo yanayohusu masuala ya haki za wanawake na watoto. Mafunzo haya yanawajengea uwezo wa kuyafuatilia na kuripoti,” amesema Olengurumwa.
Olengurumwa amesema kuwa, katika mafunzo hayo watapata nafasi ya kutoa maoni yao juu ya kutatua changamoto za kimahakama, kwa wataalamu wanaofanya mapitio ya changamoto hizo, pamoja na kujipanga katika kuweka mikakati ya kufanya kazi na Serikali pamoja na wadau wengine katika kutetea haki za binadamu.

Leave a comment