POLISI nchini Uganda imemkamata mshitukiwa Kiongozi Mkuu na Mratibu wa Kubdi la Waasi la Allied Democratic Forces (ADF) leo tarehe 15 machi 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, … (endelea).
Kwamujibu wa Msemaji wa Polisi Fred Enanga amesema kuwa Abdallh Kapanda Musa ,Maarufu kama Mogo , alikamatwa katika eneo la kati mwa Uganda akidaiwa kupanga shambulio dhidi ya Mashirika ya usalama na watu mashuhuri.
Alisema Bunduki iliyokuwa na risasi, simu 11 na kifaa cha kuhifadhi taarifa za kujihadi zilipatikana wakati wa msako uliofanyika nyumbani kwa mshukiwa huyo.
Hata hivyo Mashirika ya Usalama yanamshuku mshitakiwa kuwa sehemu ya kundi lililopanga mashambulizi dhidi ya kituo cha Polisi cha Central mjini Kampala mnamo Novemba mwaka jana .
Mashambulio hayo yalipelekea jeshi la Udanda kuvuka mpaka na kuingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupambana na wanamgambo hao wenye mafungamano na wanamgambo wa wa kundi la kigaidi la Islamic State [IS]
Leave a comment