Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara Tanzania, Zambia zakubaliana kutatua changamoto za kibiashara
BiasharaHabari Mchanganyiko

Tanzania, Zambia zakubaliana kutatua changamoto za kibiashara

Spread the love

Tanzania na Zambia zimekubaliana kutatua changamoto nane kati ya 24 za kibiashara na 16 zilizobaki zimewekewa utaratibu wa kuzitatua ifikapo tarehe 31 Disemba 2023 ili kurahisisha ufanyajibiashara  baina ya nchi hizo ikiwemo kupunguza msongamano wa malori katika mpaka wa Tunduma. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia, Lillian Bwalya wakitia saini Makubaliano ya kutatua changamoto za kibiashara 8 kati 24 kati ya Tanzania na Zambia wakati wa Mkutano wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika 09 – 10/10/2023 katika Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani- Tunduma, Songwe. Vikwazo 16 vitatatuliwa kabla ya Disemba 2023.


Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdallah juzi Jumatano wakati akizungumza na vyombo vya habari baada ya Mkutano wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara kati ya Tanzania na Zambia uliofanyika  tarehe 9 na 10 mwezi huu katika Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani- Tunduma, Songwe.

Aidha, Dk. Abdallah amesema nchi hizo zimekubaliana kuwa bidhaa zinazosafirishwa kutoka Tanzania kwenda nchi nyingine kupitia Zambia zikiwa na vibali vyote vinavyohitajika ziruhusiwe kupita nchini humo  kwenda nchi husika bila kizuizi kulingana na Makubaliano ya Kibiashara chini ya Shirika la Biashara la Dunia (WTO) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Vilevile, amezitaka Taasisi zote za umma zinazohusika na utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara wa huduma ya usafirishaji baina ya nchi hizo kuhakikisha hawawakwamishi bila sababu za msingi bali kuwasaidia kutatua changamoto zao hususani upatikanaji wa vibali kulingana na Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika makubaliano ya kibiashara chini ya Shirika la Biashara la Dunia na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (wa nne kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara (Watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Bw. Elijah Mwandumbya ( Watatu kulia) wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia, Lillian Bwalya (wa pili kushoto) pamoja na wajumbe wengine katika picha ya pamoja baada ya kutia saini Makubaliano ya kutatua changamoto za kibiashara kati ya Tanzania na Zambia Wakati Mkutano wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika 09 – 10/10/2023 katika Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani- Tunduma, Songwe.

Katika kuhakikisha masuala hayo yanafanikiwa, Dk. Abdallah ametoa rai kwa wafanyabiashara ya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kuhakikisha wanapata vibali vyote vinavyohusika kabla ya kuanza safari ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa hizo bila vikwazo na kuzifikisha katika nchi husika kwa wakati.

Katika hatua nyingine ya makubaliano yaliyotiwa saini na pande zote mbili, amesema Serikali ya Tanzania imekubali kufanya mapitio na marekebisho ya Tozo ya Maendeleo ya Reli kama inavyotekelezwa katika Itifaki ya Biashara ya SADC na  kuharakisha mchakato wa urazinishaji wa kanuni za usafirishaji ili ziendane na kanuni za usafirishaji zinazotekelezwa katika Eneo Huru la Biashara la Utatu (Tripatite transport regulations).

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia, Lillian Bwalya amesema nchi ya Zambia imekubali kutatua changamoto hizo ili kurahisisha na kukuza biashara za mpakani baina ya nchi hizo.

Akitaja baadhi ya makubaliano yaliyotiwa saini baina ya nchi hizo, amesema Zambia imekubali kuboresha changamoto za miundombinu ikiwemo upanuzi wa barabara na kutekeleza mfumo wa upatitanaji wa vibali kabla ya kufika mpakani ili kuboresha mtiririko wa magari mpakani na kuondoa msongamano wa magari uliopo mpakani Tunduma.

Aidha, amesema Zambia imekubali kutumia mfumo wa ufuatiliaji wa mizigo kwa njia ya elektroniki unaotekelezwa nchini Tanzania, au kuharakisha mchakato wa ununuzi wa mfumo unaopendekezwa kutumiwa na Mamlaka ya Mapato ya Zambia (ZRA).

Vilevile, Zambia imekubali kuharakisha urazinishaji wa ada na tozo za  barabara kwa Dola za Marekani 10 kwa kilomita 100 unaotekelezwa kaitika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Bwalya pia amesema Zambia imekubali kuangalia uwezekano wa kutumia mfumo wa kisasa wa ufuatiliaji wa magari barabarani ili kuondoa na kupunguza vizuizi vya ukaguzi barabarani.

Vilevile, Zambia imekubali kutumia Ofisi jijini Dar es Salaam inayotolewa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya Maafisa wa uondoshaji wa mizigo ya Zambia kuanzia Desemba 31, 2023 ili kirahisisha usafirishaji wa mizigo na kuondoa msongamano wa magari mpakani.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema makubaliano hayo ni muhimu katika kutatua changamoto mbalimnali baina ya nchi hizo hususani katika kupunguza msongamano wa malori katika mpaka  wa Tunduma unaopitisha asilimia 80 ya mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi za kusini mwa Afrika zisizo na bahari.

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi), Elijah Mwandumbya  akishiriki mkitano huo amesema tozo na kodi mbalimbali zitaendelea kupitiwa na kurekebishwa ili kuwezesha sekta binafsi kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza kutokana na makubaliano hayo ili kukuza biashara na uchumi wa Taifa

Naye Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule amesema changamoto zilizoondolewa zitaongeza ufanisi wa utoaji huduma na kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!