Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye, Kubenea wapeta Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Sumaye, Kubenea wapeta Chadema

Frederick Sumaye, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema. Picha ndogo, Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu na Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo wameibuka nafasi tofauti za uongozi wa Chadema Kanda ya Pwani walizokuwa wakiwania, anaandika Charles William.

Sumaye alikuwa akiwania nafasi ya mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, huku Kubenea akiwania kuwa makamu mwenyekiti wa kanda hiyo.

Uchaguzi huo ambao wapiga kura wake ni wajumbe wa mkutano maalum wa Baraza la Uongozi Kanda ya Pwani umefanyi Jumapili, Machi 19, katika ukumbi wa Lamada Hotel, jijini Dar es Salaam.

Sumaye ameibuka na ushindi wa kura 74 sawa na asilimia 83 huku mpinzani wake pekee Gango Kidera akipata kura 15 sawa na asilimia 17.

Katika nafasi ya makamu mwenyekiti wa kanda hiyo, Kubenea ameshinda kwa kura 60 sawa na asilimia 67.41, Mustafa Hassanali kura 18 sawa na asilimia 20.2 huku Adolf Mkono akipata kura 11 sawa na asilimia 12.35.

Kwa upande wa nafasi ya mweka hazina, Ruth Mollel ameibuka na ushindi wa kura 50 dhidi ya Lucy Magereli aliyepata kura 20 (mbunge wa viti maalum pia) huku Florence Kasilima akiambulia kura 19.

Idadi ya wapiga kura waliotakiwa kushiriki uchaguzi huo ni 112 lakini waliojitokeza ukumbini na kipiga kura ni 89.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

error: Content is protected !!