Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Lissu aibuka kidedea TLS
Habari MchanganyikoTangulizi

Lissu aibuka kidedea TLS

Tundu Lissu, Rais wa TLS
Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ameibuka na ushindi katika nafasi ya urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) huku Godwin Simba akichaguliwa kuwa makamu wake, anaandika Charles William.

Taarifa kutoa ukumbi wa AICC Arush zinaeleza kwamba, Lissu ameibuka na ushindi huo wa asilimia 90 dhidi ya wagombea wenzake wanne akiwemo Francis Stolla, Victoria Mandari na Godwin Mwapongo.

Wakati Lissu akipata kura 1,411 kati ya 1682 mpinzani wake wa karibu Stolla aliyekuwa akijaribu kutetea nafasi ya urais wa TLS akipata kura 64, Victoria Mandari 176 na Godwin Mwapongo 64.

Kwa upande wa wajumbe wa baraza la TLS, wajumbe waliochaguliwa na mkutano mkuu wa TLS ni Jeremiah Mutobesya, Gida Lambaji, Hussein Mtembwa, Aisha Sinda, Steven Axweso, David Shilatu na Daniel Bushele.

Ushindi wa Lissu unakuja katika kipindi ambacho Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa ameonya kuwa anaweza kuchukua hatua za kuifuta TLS kwa madai kuwa imeanza kugeuka chama cha siasa.

Aidha, Rais Magufuli pia alinukuliwa akionya juu ya mpango wa chama cha siasa ambacho hakukitaja, akidai kuwa kinajipanga kumuondoa Rais wa TLS aliyepo madarakani (Francis Stolla).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

error: Content is protected !!