Monday , 4 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu St. Mary’s Mbezi Beach High School yafanya maajabu kidato cha nne
Elimu

St. Mary’s Mbezi Beach High School yafanya maajabu kidato cha nne

Spread the love

 

WANAFUNZI waliomaliza  kidato cha nne kwenye shule ya sekondari St Mary’ s Mbezi Beach na kufaulu kwa daraja la kwanza wamepewa zawadi mbalimbali kama motisha kwa wanafunzi wengine kuendelea kufanya vizuri kitaaluma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hafla ya kuwapongeza wanafunzi hao ilifanyika jana kwenye maeneo ya shule hiyo, Mbezi Beach na kuhudhuriwa na wazazi na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne.

Zawadi walizopewa wanafunzi hao ni pamoja na fedha taslim, nguo za michezo pamoja na vitabu mbalimbali vya kitaaluma.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu Mkuu wa shule hiyo, Rajab Balele, alisema mwaka 2020 walimu waliahidi kuleta mageuzi makubwa na walipambana usiku na mchana na kufanikiwa kupata matokeo mazuri.

Alisema wanafunzi 106 wa shule hiyo walihitimu kidato cha nne mwaka jana na miongoni mwao, wanafunzi 29 walipata daraja la kwanza, daraja la II wanafunzi 35 wanafunzi 13 daraja la tatu na kwamba hakuna aliyepata sifuri.

“Walimu kwa kushirikiana na wanafunzi wamefanyakazi kubwa sana usiku na mchana kuwa wabunifu kufundisha mpaka wanafunzi wengi kufaulu kwa alama za juu,” alisema na kuongeza.

“Nilipopata matokeo yetu ya kidato cha nne kwa kweli nilichanganyikiwa kwasababu sikuwa natarajia kwamba tutafaulisha kwa kiwango kikubwa namna hii, tulilahidi kufanya vizuri lakini matokeo yamekuwa mazuri sana kuliko nilivyotarajia,” alisema.

Balele aliwataka wanafunzi hao wasibweteke na badala yake waendelee kufanya vizuri kwenye elimu ya kidato cha tano na sita ili kupata alama zitakazowawezesha kujiunga na vyuo vikuu bila vikwazo.

“Kuna wakati shule ilikuwa hadi daraja 0 wanafikia wanafunzi 62 lakini kwa sasa hakuna division  0, na daraja la kwanza wameongezeka huu ndo mwaka tumefanikiwa kupata divisheni one nyingi kuliko mwaka wowote,” alisema na kuongeza.

“Kuna kufaulu na kufaulu sana, kwa hiyo ukiangalia matokeo yetu ya mwaka huu darala la kwanza za kiwango cha juu tumezipata nyingi na huo ndio utakuwa mwendo wetu tutahakikisha hakuna daraka 0 miaka yote na daraja la kwanza zitaendelea kuongezeka,” alisema.

Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Shadrack Mgaya, alisema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kitaaluma.

Alisema mafanikio ya wanafunzi yanategemea pembe tatu ambazo ni mwalimu, mwanafunzi na mzazi ambapo kila mmoja anapotimiza wajibu wake matokeo yanakuwa  mazuri kama ambayo shule hiyo imepata kwa kidato cha nne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo

Spread the loveMwalimu Mkuu wa shule msingi Hanihani, kata ya Igunga wilayani...

ElimuHabari za Siasa

Prof Muhongo ataka ubunifu mitaala mipya ya elimu

Spread the loveSERIKALI imetakiwa kuhakikisha  maarifa, ujuzi, uvumbuzi na udadisi vinazingatiwa kwenye...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa saidizi kwa walimu, wanafunzi wenye ulemavu Ilala

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi msaada wa vifaa saidizi kwa walimu...

ElimuHabari Mchanganyiko

CBE yaanza kutoa mafunzo wahudumu wa mabasi

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimeanza kutoa mafunzo kwa...

error: Content is protected !!