Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Spika Tulia awapa kipimo cha mavazi wabunge
Tangulizi

Spika Tulia awapa kipimo cha mavazi wabunge

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson amewakumbusha wabunge kuzingatia uvaaji wa mavazi yanayoruhusiwa kikanuni na kuwa tayari kwa jambo lolote ikiwemo kwenda Ikulu kuapishwa kama itatokea hivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Dk. Tulia ametoa agizo hilo leo Ijumaa, tarehe 11 Februari 2022, bungeni jijini Dodoma akisema, suala hilo huwa halipendwi kuzungumza lakini linakuwa na tija katika uendeshaji sahihi wa shughuli za muhimili huo kwa mujibu wa kanuni walizojiwekea.

“Kanuni zimetuwekea kipimo, lakini kipimo kingine unacho wewe, kabla hujaja humu bungeni wakati unajiandaa wewe jiambie kama umeitwa na Rais kuapishwa umeteuliwa jambo, ndio utoke humo ndani uende Chamwino utakwenda au utaomba kwenda nyumbani kwanza,” amehoji Dk. Tulia

“Hicho ndio kipimo rahisi, ikiwa waziri mkuu kapigiwa simu kwamba mlete fulani nataka kumwapisha kwa nafasi fulani, utamwomba uende kwanza nyumbani au utakwenda moja kwa moja? Kama huwezi kwenda moja kwa moja basi ujue vazi hilo humu ndani haliruhusiwi,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!