Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lataka muongozo usafishaji mito
Habari za Siasa

Bunge lataka muongozo usafishaji mito

Spread the love

 

BUNGE la Tanzania, limeishauri Serikali, kuandaa muongozo wa kitaifa wa usimamizi wa usafishaji mito, ili kutunza mazingira. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ushauri huo leo Ijumaa, tarehe 11 Februari 2022, bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mwakiposa Kihenzile, akisoma taarifa ya shughuli za kamati hiyo kuanzia Januari 2021 hadi Februari mwaka huu.

Ushauri huo umetolewa baada ya kamati hiyo, kujadili taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, kuhusu Mwongozo wa Usimamizi na Usafishaji Mito katika Jiji la Dar es Salaam, pamoja na mikakati ya Serikali kwenye kuanisha maeneo ya uchimbaji mchanga nchini.

“Kamati ilielezwa kuwa muongozo huo ulianzishwa kwa lengo la kupunguza madhara yanayoweza kutokana na uchimbaji holela wa mchanga, katika mito ya Dar es Salaam. Madhara yanayotazamiwa ni pamoja na mmomonyoko wa kingo za mito, mafuriko, uharibifu wa miundo mbinu, mali na hata uhai wa watu na viumbe hai wengine,” amesema Kihenzile.

Kihenzile amesema, kamati hiyo inaishauri Serikali iandae mwongozo utakaotumika nchi nzima, ili kuepuka athari za uharibifu wa mazingira.

“Mwongozo huu ni wa mwaka 2019 na unatumia Dar es Salaam, kama eneo la mfano. Kwa kuwa umeshatekelezwa kwa miaka miwili sasa, Kamati inaishauri Serikali kuandaa mwongozo wa nchi nzima na kuanza utekelezaji katika maeneo mengine tusisubiri mpaka na yenyewe yakaathirika zaidi,” amesema Kihenzile.

Wakati huo huo, kamati hiyo imeishauri Serikali kuongeza idadi ya madampo kwenye Jiji la Dar es Salaam, pamoja na viwanda vya kuchakata taka, ili kutokomeza tabia ya baadhi ya wananchi kutupa takataka katika mito.

“Kwa sasa Dar es Salaam lina dampo la kisasa moja tu, ambapo ni changamoto kwa takataka za jiji zima kuweza kufikishwa katika dampo hilo, jambo linalopelekea baadhi ya wananchi waliokaribu na mito kutupa takakata katika mito. Kamati inaisisitiza Serikali kuja na mkakati wa kujenga madampo kulingana na ukubwa wa Jiji la Dar es Salaam,” amesema Kihenzile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!