Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Spika Ndugai: Waiteni NIDA… kuna hela zimeliwa
Tangulizi

Spika Ndugai: Waiteni NIDA… kuna hela zimeliwa

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano nwa Tanzania, Job Ndugai ameiagiza Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kuwaita viongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa  (NIDA) na kuwahoji ili kujua nini kinachoendelea kwani wabunge wanahisi kuna hela zimeliwa. Anaripoti Gabriel Mushi … (endelea)

Amesema NIDA hawafanyi kazi nzuri hivyo kupitia kamati hiyo waitwe ili kieleweke.

“Tumeanza nao kitambo sana ni kiswahili tu, kupitia kamati tutajua nini kinaendelea huko Nida, ndio maana labda mbunge anahisi kuna hela zimeliwa,” amesema.

Spika Ndugai ametoa agizo hilo leo tarehe 2 Novemba, 2021 bungeni jijini Dodoma baada ya Mbunge wa Makunduchi Ravia Idarus Faina  kuhoji kwanini uzalishaji na usambazaji wa vitambulisho vya Taifa umepungua licha ya NIDA kuongezewa mashine mbili za kuzalisha vitambulisho hivyo.

Aliongeza NIDA hawaoni wametumia fedha za wananchi vibaya sana.

Akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Khamis Hamza Chilo alikiri kuwa NIDA ilikuwa na mashine mbili ambazo zilizalisha vitambulisho vichache ikilinganishwa na mahitaji, lakini waliomba fedha serikali na kuongeza mashine nyingine mbili ambazo sasa shughuli za usajili, utambuzi na utoaji wa vitambulisho hivyo unaendelea vizuri.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Amesema hadi kufikia tarehe 12 Oktoba, 2021 NIDA walikuwa wameshazalisha vitambulisho karibu milioni 10 ambavyop vipo tayari  na muda wowote vitakwenda kusambazwa kwa wananchi.

“Kuhusu kutumia fedha vibaya, hakuna fedha iliyoingia katika kaunti ya NIDA aidha, kutoka ndani ya serikali au wafadhili ikatumika vibaya, hivyo nimwambie Mbunge kwamba fedha zote zimetumika in accordingly,” amesema.

Katika swali la msingi, Mbunge huyo alihoji ni lini Serikali itajenga Ofisi za NIDA katika Wilaya ya Kusini Unguja.

Naibu Waziri huyo wa Mambo ya Ndani alijibu kwamba Ofisi ya Nida katika wilaya ya Kusini Unguja mkoa wa Kusini itajengwa katika nwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema katika kuhakikisha huduma hiyo ya vitambulisha inasogezwa karibu na wananchi,  tayario NIDA imefungua ofisi 150 katika wilaya zote za Tanzania bara na Visiwani.

1 Comment

  • Hili bunge na hao NIDA wote ni wapiga hela tu. Bunge hili si halali. Na NIDA huu mwaka mzima tangu nipewe namba ya kitamvulisho lakini kitambulisho hakipo mpaka leo. Wizi na ubadhirifu tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!