Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Mbeya akoshwa na jitihada za Benki ya Exim kuwahudumia wafanyabiashara
Habari Mchanganyiko

RC Mbeya akoshwa na jitihada za Benki ya Exim kuwahudumia wafanyabiashara

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Mbeya iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Spread the love

 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera  ameonyesha kuridhishwa na huduma pamoja na jitihada za Benki ya Exim katika kuwahudumia wafanyabiashara na wateja wengine wa benki jijini humo huku akionesha kuvutiwa zaidi na riba nafuu inayotolewa na benki hiyo kwa wateja wake. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Homela aliezea kuridhishwa huko na huduma za benki hiyo alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki ya Exim mkoani wa Mbeya iliyoandaliwa na benki hiyo ili kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

“Baada ya kufuatilia vizuri huduma za Benki ya Exim nimebaini kuwa ni huduma rafiki zaidi kwa wafanyabishara na wajasiriamali na zaidi nimevutiwa na kiwango cha riba kinachotozwa kupitia mikopo yao ambacho hakimuumizi mkopaji. Binafsi nimevutiwa zaidi na akaunti ya watoto pamoja na akaunti wa akiba na kudhihirisha hili nipo tayari kufungua akaunti hizi ili niweze kufurahia huduma hizi,’’ alisema.

Hafla hiyo ilihudhuliwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na  Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Matundu alisema, kupitia tukio hilo muhimu  walilenga pia  kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja sambamba na kutoa kwa wateja hao kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Mbeya wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

“Kupitia hafla hii pamoja na mambo mengine tupo hapa kuwafahamisha wateja wetu kuhusiana na maboresho ya huduma zetu mbalimbali kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidigitali na kuwarahisishia utoaji wa huduma zetu.’’ alisema Bw Matundu.

Alisema hali ya uchumi katika mkoa huo inatoa fursa kubwa ya ukuaji kwa benki hiyo na hiyo ndio sababu imejipanga  kuhudumia wateja  Wakubwa, Wadogo na wa Kati  ili kuleta ustawi kwenye sekta muhimu kwa mkoa huo ikiwemo biashara, kilimo na ufugaji .

“Takwimu zinaonyesha Mkoa wa Mbeya umeendelea kujenga uchumi imara na endelevu, na hivyo ufanisi katika mfumo wa fedha ni moja ya mahitaji ya muhimu na ya msingi katika ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla. Benki ya Exim tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha hilo pamoja ’’ alisema

Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (Kushoto) akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera (Kulia) alipokuwa akiingia hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo aliwatoa hofu wateja wa benki hiyo mkoani humo kuendelea kuiamini benki hiyo kwa kuwa imeendelea kujitanua zaidi hadi nje ya mipaka ya nchini ikiwemo katika mataifa ya Uganda, Ethiopia, Comoro na Djibouti, hatua ambayo inatoa fursa kwa wafanyabiashara kutafuta fursa za kibiashara nje ya nchi wakiwa na uhakika wa huduma za benki hiyo.

“Ni kupitia kujitanua kwetu huku hadi nje ya mipaka ya nchi ndio sababu tunawakikishia wateja wetu kwamba hakuna haja ya kujifungia ndani ya mipaka yetu ni wao tu kufungua milango hadi nje ya mipaka kwasababu Exim tupo nao hadi nje ya mipaka’’

Maofisa waandamizi wa Benki ya Exim wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (Katikati) pamoja Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (Kushoto) wakisalimiana na wateja wa benki hiyo mkoa wa Mbeya wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

“Zaidi, tumejipanga kuhakikisha Benki inafanya vizuri  kwa kuweka kipaumbele katika uboreshaji wa namna ya kupata na kutumia huduma zetu. Tunataka upatikanaji na utumiaji wa huduma za Benki ya Exim uwe rahisi, huku tukiendelea kusizogeza huduma hizo karibu zaidi na wateja wetu.’’ Alisema.

Kwa upande wao wateja wa benki hiyo, walionyesha kuridhishwa na huduma za benki hiyo ambapo pamoja na kuipongeza kwa jitihada zake za kujitanua nje ya mipaka ya nchini bado waliiomba ione umuhimu kufungua matawi yake katika nchi za Zambia na Malawi ili kutokana na wao kuwa na ukaraibu zaidi wa kibiashara na mataifa hayo, ombi lililopokelewa vema na uongozi wa benki hiyo na kuahidi kulifanyia kazi.

1 Comment

  • Hii benki ya Exim siyo benki ya Tanzania.
    Kwa nini inaruhusiwa kushika uchumi wa nchi yetu?
    Ukweli hatuna tawi kwao. Hii siyo haki wala usawa. Ulaya hawaruhusu zaidi ya tawi moja kwa benki za nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

error: Content is protected !!