November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Conte amrithi Nuno Spurs

Spread the love

 

ANTONIO Conte, kocha raia wa Itary aemeingia kandarasi ya miaka miwili kukinoa kikosi cha Tottenham Hotspurs inayoshiriki Ligi Kuu nchini England mara baada ya kuchukua nafasi ya Nuno Espirito Santo aliyetimuliwa hivi karibuni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Conte amerejea tena nchini Uingereza siku chache mara baada ya Spurs kumfurusha kocha wao, kufuatia kipigo cha mabao 3-0, walichokipata dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo

Kocha huyo ambapo hapo awali ilitajwa kujiunga na Mancheaster United, mara baada ya kocha wa sasa wa klabu hiyo Ole Gunner solskjaer Kuonekana kuwa katika wakati mgumu kufuatia kupata matokeo mabovu.

Mpango huo haukutimia mara baada ya solskjaer kuaminiwa na bodi ya klabu ya Manchester United na hivyo kuendelea na kibarua chake ambapo kesho atakuwa ugenini nchini Itary, kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, dhidi ya Atalanta.

Akifunguka mara baada ya kuingia kandarasi yake na Tottenham, Conte alisema kuwa ilikuwa mapema sana kwake kurejea kufundisha mara baada ya kuachana na klabu ya Inter Milani inayoshiriki Ligi Kuu nchini Itary

“ Sikuweza kujiunga na Tottenham kwenye majira ya kiangazi kutokana na kwamba ilikuwa mapema kurejea kufundisha baada ya kuachana na Inter Milan.” Alisema kocha huyo

Hii ni mra ya pili kwa Conte kurejea nchini Uingereza, mara baada ya kukinoa kikosi cha Chelsea katika kipindi cha miaka miwili kuanzia msimu wa 2016 mpaka 2018 na kufanikiwa kuwapa taji moja la Ligi Kuu.

 

error: Content is protected !!