December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai kuwaapisha wabunge ACT-Wazalendo

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai leo Jumanne tarehe 15 Desemba 2020, atawaapisha wabunge wanne wa ACT-Wazalendo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge imesema, wabunge hao wataapisha saa 10 jioni katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020, ACT-Wazalendo kilishinda majimbo manne ya Pemba visiwani Zanzibar.

Walioshinda ni; Hatibu Said Haji (Konde), Salum Mhamed Shafi (Chonga), Omar Ali Omar (Wete) na Khalifa Mhamed Issa wa Mtambwe.

Wabunge wateule wanakwenda kuapishwa baada ya chama hicho kuwaruhusu wanachama wake wote walioshinda udiwani, ubunge na uwakilishi kwenda vyombo vya uwakilishi ili kuapishwa na kuanza kuwatumikia wananchi.

error: Content is protected !!