November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai: Bunge limemlipa Lissu mamilioni

Tundu Lissu, Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri, ameueleza umma kuwa, Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amelipwa Sh. 250 milioni na taasisi hiyo (Bunge). Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Ndugai ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Januari bungeni huku Lissu akisisitiza kwamba, akisisitiza kuwa hajawai kupata huduma ya matibabu kutoka Ofisi ya Bunge.

Muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu Spika Ndugai alisema kuwa, “ninayo mambo ya kusema juu ya uzushi ambao unaendelea kuwa, tangu Lissu aliposhambuliwa Ofisi ya Spika haijawai kumpatia stahiki yake ya matibabu.”

Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu Spika Ndugai alianza kusema “sasa kipindi cha maswali na majibu kimeishatolewa na nimemaliza matangazo. Kuna jambo ambalo nataka kulisemea na nilikuwa nikikataa kulisema  tangu mwanzo, linamhusu Tundu Lissu. Kwa sasa tumeamua kwenye ofisi yetu kuanza kujibu kwa kuwa nilikuwa nikikataa sana kujibu.

“Tangu mwanzo kwa sababu tulikwa tunaamini kuwa, bado yupo kitandani na haipendezi watu wazima kubishana na mgonjwa.”

Spika Ndugai amesema, kutokana na mazingira ya sasa Bunge linalazimika kujibu tuhuma zinazovurumishwa na Lissu.

” Lakini sasa dalili zote zinaonesha akiongea lazima tujibu, maana kama mtu anaamua kufanya ziara duniani ima kuwa anaelewa anachokiongea.

“Lakaini mwanzo unaweza kuhisi kwamba katika kuugua kunakuwa na baadhi ya mambo ambayo yanafanywa yanakuwa yamempita.

“Moja ya madai yake makubwa ni kuwa Bunge hili halijawahi kumpa wala kumjali kifedha tangu apate matatizo Septemba 7 mwaka 2017.”

Spika Ndugai pamoja na kauli hiyo, amesema anaendelea kumpa pole Lissu kutokana na yale yaliyomkuta na kwamba, sasa Bunge litaendelea kutoa ufafanuzi kadiri siku zinavyoenda.

“Lakini itoshe tu kusema kwa Watanzania kwamba, Bunge hili kupitia ofisi yangu toka Septemba 7, 2017 hadi Desemba bila kujumuisha za Januari kupitia ofisi yangu, tumeshamlipa Lissu malipo mbalimbali ya jumla ya sh, milioni 207.

“Ukijumlisha na michango yenu kwa ajili ya matibabu ambayo tulilipa katika Hospitali ya Nairobi alikolazwa (milioni 43) ukijumlisha pamoja unapata milioni 250,” amesema Spika Ndugai na kuongeza;

“Unapoendelea kusema kila mahali kwamba, Bunge hili halijawahi kutoa hata senti moja kwa ajili yake katika jambo hili, ni jambo la uongo, uongo.. uongo kabisa.

“Haliwahusu hili…. Nalitupa upande wake ili akanushe ili nije na mkeka wa mambo yooote” amesema Ndugai.

Lissu mara kadhaa amekuwa akisema kwamba, Ofisi ya Bunge imemtelekeza kwa kuwa, haijampa stahili zake za matibabu licha ya sheria kuelekeza hivyo.

https://www.youtube.com/watch?v=rKlyfGh-TCE&feature=youtu.be

error: Content is protected !!