Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto ‘akoga’ mashambulizi ya Spika Ndugai 
Habari za Siasa

Zitto ‘akoga’ mashambulizi ya Spika Ndugai 

Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo leo tarehe 31 Januari 2019 ‘amekoga’ mashambulizi ya moja kwa moja kutoka kwa Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Spika Ndugai alimshambulia Zitto ndani ya ukumbi wa Bunge jijini Dodoma kwamba amezoea kusema uongo. Amemtaka mbunge huyo kijana kujirekebisha.

Ndugai amemwambia Zitto kwamba anamweka kiporo kuhusu madai ya ubadhirifu wa Sh. trilioni 1.5 zinazotajwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2016/17.

Ndugai amesema kuwa, Zitto ni muongo na wakati wa kumpeleka katika Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge sio sasa, lakini atafika huko.

Pia Spika Ndugai alimshambulia Zitto kwa madai ya kuandika uongo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram jana Jumatano asubuhi, muda mfupi baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu.

“Huyu Zitto aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kwamba CAG alikuwa amefanya ukaguzi Hazina na katika ukaguzi huo aligundua wizi mkubwa, ubadhirifu wa trilioni 1.5 na ametoa ripoti maalumu ya ukaguzi huo na ripoti hiyo imefika Ofisi ya Spika na Spika amekalia ripoti hiyo.

“Sasa hayo mengine nilikuwa siyajali sana kuhusu mimi kwa mfano kuhutuhumiwa kwamba nimekalia ripoti hiyo na hasa kwenye Instagram ya tarehe 8 (Januari 2019), ningependa kusema mbele ya Bunge hili na kwa wananchi wa Tanzania kwamba ndugu yetu Zitto anapenda sana tabia za kusema uongo na haipendezi mtu mzima kusema uongo huo, sio utamaduni wetu.”

Akioneshwa kukasirishwa na kitendo hicho, Spika Ndugai amesema kama hiyo barua imetoka kwa CAG na imeenda kwa Spika wakati ambao wabunge walikuwa likizo, Zitto alijuaje wakati hafanyi kazi Ofisi ya Spika wa Bunge wala Ofisi ya CAG.

“Wewe (Zitto) unajuaje pale katikati, unafanya kazi Ofisi ya CAG au inakuwaje? Lakini niseme tu kwamba barua tajwa yeye alisema tarehe 8, mimi nimeletewa Ofisi ya Dar es Salaam tarehe 16 mwezi huu (Januari), kwa hiyo haikuwa kweli, lakini pia baada ya kuipata tarehe 16 muda mfupi baadae nikawa nimeipeleka kwenye Kamati ya PAC (Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali) kama ilivyo ada, kwa sababu hata ninyi wenyewe ubadhirifu wa shilingi trilioni 1.5, hivi Spika anakaliaje?”alieleza Ndugai

Kwa mujibu wa Spika Ndugai, kama Bunge hilo hilo lilihangaika na hoja ya Zitto katika sakata lililohusu upigaji wa fedha katika akaunti ya malipo ya nje (Escrow) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zaidi ya Sh. bilioni 300 za Escrow, leo Sh. trilioni 1.5 Spika anawezaje kuzikalia.

Ndugai amesema kitendo hicho cha Zitto kuandika uongo, huko sasa ni kupakana matope na taifa zima linamwona Spika kama ni mtu wa ajabu ajabu.

“Na haya yanatokana na ninyi wenyewe wabunge kuipaka matope ya kila aina ofisi ya spika. Sasa sijui kwa madhumuni gani, sujui kama ni ku-retaire imprest, kwa hiyo niseme kwamba taarifa hiyo haikuwa ya kweli ni taarifa ni ya uongo,”amesisitiza Ndugai.

Aliwaleza Wabunge kwamba kama wanavyojua tarehe 20 Aprili mwaka 2018, Rais John Magufuli alikuwa wakati anawaapisha Majaji, Ikulu Dar es Salaam alimuuliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwamba alipomsomea taarifa hiyo kabla hajaipeleka Bungeni,  hakumwambia habari ya wizi wa sh. trilioni 1.5, kwamba hizo hela zimeibiwa.

Katika kusisitiza hilo, Ndugai amesema “ninyi wote mliosikiliza CAG alimjibuje pale, kasema hakuna mambo kama hayo mbele ya Rais, Ikulu.

Na wiki iliyopita nilipeleka jambo hili kwenye kamati ya PAC na iliulizwa pia kama kuna wizi wa aina hiyo, yeye mwenyewe akiwepo CAG, Deputy CAG (Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) akajibu hakuna wizi wowote wala ubadhirifu wa trilioni 1.5.”

Kutokana na hali hiyo, Spika Ndugai alitoa ushauri wake kwa Wabunge kwa ujumla wake kwamba ni vyema wakajikita katika ushindani wenye tija sio kuendesha siasa zisizokuwa na maana na kutoa taarifa zinazoenda dunia nzima kama vile kuna jambo fulani, hilo ni jambo ambalo halina tija.

“Leo natoa tu kwa watanzania wajue katika hili Zitto ni mwongo, na akitaka nimfanyie ytafiti wa mengine ya uongo wa ambayo ameyasema yapo ya kutosha, badilika, badilika ndugu yangu mbona mimi sijawahi kukusingizia, hujisikii vibaya yaani kwenye moyo wako?,”amesema Spika Ndugai.

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

Habari za Siasa

Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania

Spread the loveUSHINDI wa aliyekuwa mgombea  urais wa upinzani nchini Senegal, Bassirou...

error: Content is protected !!