August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai amtupa ‘jela’ Mnyika, Wapinzani wasusa

John Mnyika, Mbunge wa KIbamba (kushoto). Kulia ni Job Ndugai Spika wa Bunge

Spread the love

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameamuru askari wa Bunge wamtoe nje, John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na iutohudhuria vikao saba la bunge hilo vinavyoendelea, anaandika Dany Tibason.

Ndugai amechukua maamuzi hayo kwa kile alichokiita ni utovu wa nidhamu uliofanywa na Mnyika kwa kubishana na kiti baada ya kutokea malumbano kati yake na spika.

Baada ya Ndugai kumwamuru Mnyika atoke nje aligoma kutii amri hiyo ndipo askari wa Bunge alipoingia na kumbeba juu juu na kumtoa nje ya viwanja vya Bunge, hali iliyosababisha wabunge wote wa upinzani kutoka nje na kususia kikao hicho.

Hali hiyo ilitokea baada ya Mnyika kuomba muongozo wakati Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akichangia mjadala uliokuwa unaendelea bungeni.

Mnyika aliingia katika mgogoro na Spika Ndugai baada ya kuibuka sauti kutoka kwa wabunge wa CCM aliyemwita mwizi, ndipo alipomwomba spika aamuru aliyetoa kauli hiyo afute kauli yake lakini aligoma kufanya hivyo.

Ndugai aligoma kumwamuru aliyetoa sauti hiyo afute kauli kwani alisema alitoa muda kwa Lusinde na Mnyika hivyo huyo mwingine hayupo katika mamlaka yake kwa wakati hiyo, kitendo ambacho kilipingwa vikali na Mnyika na kuibua sintofahamu hiyo.

Katika hatua nyingine Kamati ya Maadili itakutana kumjadili Mbunge Esther Bulaya kwa kuhamasisha wabunge wenzake wa upinzani kutoka nje ukumbi wa Bunge wakati mjadala unaendelea.

error: Content is protected !!