December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai ampigia kampeni Rais Magufuli

Rais John Magufuli (kulia) akiteta jambo na Spika wa Bunge, Job Ndugai

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge ameanza kumwombea kura Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akiwa kwenye mkutano wa hadhara kwenye ziara ya Rais Magufuli mkoani Dodoma, Spika Ndugai amesema kuwa wakazi wa jimbo la Kongwa analoliongoza yeye (Spika Ndugai), wanasubiri mwaka 2020 wampe shukrani mwenyekiti wake (Dk. Magufuli).

Mwaka 2020 kunatarajiwa kufanyika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo tarehe 17 Julai 2019, katika mkutano wa Rais Magufuli na wananchi wa Wilaya ya Kongwa, mkoani humo.

Spika Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, amesema wananchi wa mkoa huo watatumia sanduku la kura kutoa shukrani zao kwa Rais Magufuli.

Aidha, Spika Ndugai amesema CCM mkoani Dodoma imejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu wa 2020, chama hicho kinashinda kwa kishindo.

“Sisi tunachosubiri 2020, sanduku la kura ili tukuonyeshe shukrani zetu kwako, kwa niaba ya CCM na kipekee. Mwenyekiti wa mkoa tumejipanga tunaelekea 2020 Mkoa wa Dodoma utakua wa kwanza kitaifa,” amesema Spika Ndugai na kuongeza:

“Dodoma imeshachukua nafasi ya kwanza na hatutaiachia hiyo nafasi ya kwanza. Vijana wangu wote wamejiandaa vya kutosha.”

Spika Ndugai amesema wanamshukuru Rais Magufuli kutokana na jitihada zake za kuleta mageuzi ya maendeleo kwenye mkoa huo, ikiwemo katika sekta ya afya, elimu na maji.

“Kongwa ni  katika jimbo kumi bora kabisa Tanzania ambayo yalikupigia kura nyingi sana sana, na mkoa wa Dodoma ulikuwa wa kwanza kitaifa,” amesema Spika Ndugai.

error: Content is protected !!