Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Machozi yenu yataniumiza – Rais Magufuli
Habari za Siasa

Machozi yenu yataniumiza – Rais Magufuli

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amesema hawezi kuongoza nchi iliyotawaliwa na machozi pamoja na watu wanaosikitika kwa unyonge. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma leo tarehe 17 Julai 2019.

Akizungumza na wananchi hao, Rais Magufuli amesema machozi ya wananchi yatamuumiza.

“Siwezi nikatawala nchi ya machozi, machozi haya yataniumiza. Siwezi nikatawala watu wanaosikitika wako kwenye unyonge na unyonge wao uko kwenye kuonwa,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amezungumzia hatua ya Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuwafutia kesi uhujumu uchumi, polisi nane waliotuhumiwa kutorosha shehena ya dhahabu.

“Hata wale polisi walioshikwa kwa wizi wa dhahabu waliokuwa wanasindikiza kule Mwanza, hata kwa kuwaona tu unaweza ukajua kwenye macho yao. DPP naye amewaachia na mimi niliamua warudishwe kazini sababu walikuwa wameshafukuzwa,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema tukio hilo liwe fundishi kwa polisi wanaopenda kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuwaacha huru wafungwa wasiohitajika kuwepo gerezani.

 “Nilishatoa maelekezo kwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, wapitie Magereza yote wazungumze na watuhumiwa walio mahabusu ili wale ambao hawahitajiki kukaa mule waachiwe,” amesema JPM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!