September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga, Azam Matatani

Ofisi za TFF

Spread the love

SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania ‘TFF’, limepiga marufuku michezo yote ya kirafiki kwa klabu zote nchini mpaka pale itakapotoa kibali maalumu kutokana na timu hizo kutofuata masharti ya Wizara na Serikali juu ya ugonjwa wa Covid 19. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… endelea

Hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya Michezo sambamba na Wizara ya Afya ilitoa muongozo maalumu kwa klabu na wamiliki wa viwanja katika kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 baada ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika taarifa iliyotoka ndani ya Shirikisho hili imeeleza kuwa TFF itakutana na klabu za Simba, Yanga, KMC na Transit Camp ambao walicheza michezo ya kirafiki hivi karibuni ambao ilionekan kuwa na dosari kubwa katika kuchukua hatua kukabiliana na maradhi ya Covid 19.

Klabu hizo zilicheza michezo hiyo ya kirafiki ili kujiweka sawa kuelekea michezo ya Ligi Kuu inayotarajia kuendelea juni 13, 2020 sambamba na Ligi daraja la kwanza.

Hivi karibuni klabu ya Azam Fc ilicheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Transit Camp na kumalizika kwa sare, huku klabu ya Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya KMC kwa mabao 3-0, huku Simba ilicheza michezo miwili ya kirafiki ndani ya siku moja.

Mchezo wa kwanza uliopigwa asubuhi kwenye uwanja MO Simba complex Arena dhidi ya Transit Camp na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 na katika mchezo mwengine uliofanyika jioni Simba iliwakaribisha KMC na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

error: Content is protected !!