Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sima ataka ujenzi soko la kisasa Singida kutoathiri wafanyabiashara
Habari za Siasa

Sima ataka ujenzi soko la kisasa Singida kutoathiri wafanyabiashara

Spread the love

MBUNGE wa Singida Mjini, Mussa Sima ameitaka Serikali kuweka mipango imara itakayohakikisha shughuli za wafanyabiashara wanaotumia Soko Kuu la Ipembe haziathiri wakati ujenzi wa soko hilo utakapoanza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Sima ametoa kauli hiyo leo Ijumaa bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la msingi kwamba Serikali itajenga soko la kisasa Singida Mjini kukidhi mahitaji ya wananchi kwani Soko Kuu la Ipembe ni la muda mrefu na miundombinu yake ni chakavu.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya rais (Tamisemi), Dk. Festo Dugange ujenzi wa Soko Kuu la Ipembe, Mkandarasi anatazamiwa kuanza utekelezaji wa mradi ifikapo Disemba, 2024.

Aidha, amesema Serikali inatambua kuwa miundombinu ya Soko kuu la Singida Mjini lililopo Mtaa wa Ipembe ni ya muda mrefu na chakavu.

“Halmashauri ya Manispaa ya Singida iliandaa andiko la kuomba fedha ya ujenzi wa soko la vitunguu la Misuna na Soko Kuu la Ipembe ambalo limependekezwa kujengwa upya.

Kupitia Mradi wa Tanzania Cities Transforming Infrustructure and Compititivenes (TACTIC) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Soko la Vitunguu la Misuna lilipata ufadhili kwa awamu ya kwanza na shughuli za upembuzi na usanifu wa mradi zinaendelea,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amesema taratibu za ujenzi wa miradi hiyo zitazingatiwa kwa kushirikiana na taasisi zote ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao wakati wa ujenzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!