Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa BAVICHA: Samia amezima maoni ya Watz kwa kusaini sheria uchaguzi
Habari za Siasa

BAVICHA: Samia amezima maoni ya Watz kwa kusaini sheria uchaguzi

Spread the love

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA),  limelaani uamuzi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kusaini miswada ya sheria za uchaguzi pasipo marekebisho madogo ya katiba kufanyika, likidai amezika maoni ya watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Pambalu, amedai kitendo cha sheria hizo kuanza kutumika kabla ya marekebisho madogo kufanyika, kunapelekea baadhi ya maoni ya wadau kutofanyiwa kazi.

“Watanzania walisema kama muda wa uchaguzi umekaribia na hatuwezi kuwa na katiba mpya basi tuwe na marekebisho madogo kwenye maeneo yatakayosaidia kuwa na uchaguzi huru na haki na ndio ulikuwa msimamo wa Chadema na wadau mbalimbali, Rais ameamua kupuuza kwa kupitisha ile sheria,” amesema Pambalu.

Pambalu amedai kuwa, kuna baadhi ya mapendekezo ya wadau yaliyotolewa yalitakiwa kuingizwa katika katiba pamoja na kwenye sheria hivyo, hivyo kitendo cha katiba kutofanyiwa marekebisho madogo, kumepelekea maoni hayo kuzikwa.

Ametaja mapendekezo na maoni ya wadau ambayo yamezikwa kwa kutojumuishwa katika katiba na sheria, ni suala la uwepo mgombea binafsi, matokeo ya urais na maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)kupingwa mahakamani, na marufuku ya wagombea kuenguliwa kinyume cha sheria.

“Wananchi wanataka tuwe na mgombea binafsi, wanataka matokeo ya urais yahojiwe mahakamani na ndio lengo la kuwa na mabadiliko madogo ya katiba, sahihi ya Rais maana yake matokeo ya Rais hayatahojiwa mahakamani. Tulitaka mabadiliko ya katiba ili kusiwe na kuenguliwa hovyo kwa wagombea, katiba ianishe muundo wa tume ya uchaguzi,” amesema Pambalu.

Tarehe 2 Aprili 2024, akiwa bungeni jijini Dodoma, Spika Bunge, Dk. Tulia Ackson, alisema Rais Samia ameshasaini miswada ya sheria ikiwemo ya sheria za uchaguzi, uamuzi uliozifanya kuwa sheria kamili na kuanza kutumika.

Sheria zilizosainiwa na Rais Samia, ni pamoja na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba 1 ya 2024, Sheria ya Tume  Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba 2 ya 2024, Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa namba 3 ya 2024 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 4 ya 2024.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!