Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Shule zinazofanya mtihani wa dini ya Kiislam zaongezeka matokeo yatangazwa
Elimu

Shule zinazofanya mtihani wa dini ya Kiislam zaongezeka matokeo yatangazwa

Spread the love

 

IDADI ya Shule ya shule za msingi zinazofanya mitihani ya elimu ya dini ya Kiislam nchini imeongezeka kulinganisha na mwaka jana kutoka shule 3903 kwa mwaka 2022 hadi kufikia 3975 kwa mwaka 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu , Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 23 Agosti na Mjumbe wa Islamic Panel Sheikh Mussa Kundecha alipokuwa akitangaza matokeo ya mitihani wa elimu ya kiislam na lugha ya kiarabu kwa shule za msingi imefanywa Tarehe 9 Agosti kwa shule 3975 kwa Tanzania Bara na Visiwani huku mtihani wa kuhitimu madarasa ukifanyika kwa siku mbili mtawalia tarehe 12, 13 Agosti 2023 .

Sheikh Kundecha amesema kuwa Mwaka 2022 mikoa iliyoshiriki ni 25 Halmashauri 151 idadi ya shule ilikuwa 3903 idadi ya watahiniwa ilikuwa 150945.

Amesema kuwa mwaka 2023 mikoa iliongezeka kuwa 28 pamoja Visiwani Halmashauri kutoka 151 mpaka 159 idadi ya shule iliongezeka kutoka 3903 mpaka 3975 huku watahiniwa wakiongezeka kutoka 150945 mpaka 157823.

“Mikoa imeongezeka mitatu sawa na asilimia 12 Halmashauri 8 sawa na asilimia 5 idadi ya shule zimeongezeka 72 sawa na asilimia 1 idadi ya watahiniwa wameongezeka 6878 sawa na asilimia 4” amesema Sheikh Kundecha.

Amesema Mtihani ulikuwa na alama 50 kwa daraja ‘A’ mpaka ‘E’ la ufaulu ambapo mtahiniwa atahesabika amefaulu kwa kupata madaraja hayo.

Watahiniwa 139181 walifaulu kwa kupata daraja A mpaka C sawa na asilimia 88.19 ya watahiniwa wote waliopata daraja E ambalo ni chini ya ufaulu walikuwa 18591 sawa na asilimia 11.81 .

Amesema kuwa wanafunzi 2681 sawa na asilimia 1.70 kwa daraja ‘B’ 8663 sawa na asilimia 5 C 4837 sawa na asilimia 30 kwa daraja ‘D’ 79803 sawa na asilimia 50 kwa daraja la ‘E’ 18000 sawa na asilimia 11.

Shule kumi bora kwa mgawanyo wa shule zenye watahiniwa 20 au zaidi Mbagala Islamic Primary Iliyopo Dar es Salaam imekuwa kinara kwa wastani wa 49.33 huku shule kumi bora katika mgawanyo wa shule zenye watahiniwa chini ya 20 shule ya Albayan Islamic iliyokuwepo Ilala Dar es Salaam ikiongoza.

Matokeo hayo yametangazwa leo tarehe 23 Agosti 2023 na Mjumbe wa Islamic Panel Sheikh Mussa Kundecha ambapo amesema kuwa

Halmashauri 159 zilishiriki kwenye mtihani huo . Shule 23 kutoka mikoa minane ya Tanzania bara na mikoa miwili kutoka visiwani ilishiriki kwenye mtihani wa somo la lugha ya kiarabu.

Amesema kuwa kwa mara ya kwanza madrasa 17 kutoka kwenye Halmashauri 8 zilishiriki katika mtihani wa kuhitimu madarasa.

“Islamc Panel imeziunganisha madrasa zilizowahi kujiwekea utaratibu binafsi wa kufanya mitihani ili kuchagiza ushindani” amesema Kundecha.

Sheikh Kundecha amesema kuwa jumla ya wanafunzi 174709 wamesajili kufanya mtihani huo ambapo waliofanikiwa kufanya mtihani huo 157823 sawa na asilimia 90.33 . Idadi ya walioshindwa kufanya kwa sababu mbalimbali ikiwa ni 6896 sawa na asilimia 9.67

Amesema kuwa idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani wa somo la kiarabu katika shule za msingi ni 694 94.42 ikiwa waliosajiliwa 735 , walioshindwa 41 sawa na asilimia 5.58 .

Wanafunzi waliosajiliwa kwa ajili ya mitihani ya Madrasa ni 166 ambapo walio bahatika kufanya mtihani ni wanafunzi 95 sawa na asilimia 57 na wale walioshindwa kufanya mtihani walikuwa 71 sawa na asilimia 42.

Amefafanua majukumu ya Islamic Panel ni pamoja Kusimamia na kuendesha elimu ya Kiislam, na somo la Kiarabu kwa shule za msingi , sekondari na vyuo cha kati.

Mkoa wa Pwani umeibuka kinara wa mitihani ya kiarabu kwa shule za msingi kwa kupata asilimia 39.99 ukifuatiwa na Mkoa wa Manyara kwa asilimia 39. 65

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za SiasaTangulizi

Walimu 12,000 kuajiriwa mwaka huu, wa kike kupewa kipaumbele

Spread the loveKATIKA mwaka 2023/2024, Serikali inatarajia kuajiri walimu 12,000 wa masomo...

ElimuHabari za Siasa

Ukomo michango wanafunzi kidato cha tano 80,000

Spread the loveSERIKALI imesema ukomo wa michango kwa wanafunzi wanaojiunga kidato cha...

ElimuHabari Mchanganyiko

Dk. Biteko apongeza mikakati ya kuinua elimu Dodoma

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko...

ElimuHabari za Siasa

Shigongo: Nafanya masters kwa kutumia kipaji pekee

Spread the loveMbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (CCM) ameishukuru Serikali kwa kurejesha...

error: Content is protected !!