Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyejaribu kumpindua Putin afariki kwa ajali ya ndege
Habari za SiasaKimataifa

Aliyejaribu kumpindua Putin afariki kwa ajali ya ndege

Spread the love

WATU 10 wamefariki dunia leo Jumatano baada ya ndege binafsi iliyokuwa ikitokea katika jiji la Moscow kwenda St. Petersburg kuanguka huko nchini Urusi.

Vyombo vya habari vya Urusi na maofisa wa anga wamesema kuwa katika ajali hiyo pia alikuwepo mwanzilishi wa kundi binafsi la kijeshi la Urusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin.

Hata hivyo, Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Urusi, Rosaviatsia imesema licha ya kwamba jina lake lilikuwa kwenye orodha ya abiria wa ndege hiyo, lakini haikufahamika mara moja kama alikuwa ndani ya ndege hiyo wakati inapata ajali.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo ni mali ya Prigozhin, ambaye aliongoza uasi mwezi Juni dhidi ya jeshi la Urusi.

Hapo awali, kituo cha Telegram kinachohusishwa na Wagner, Gray Zone kiliripoti kwamba ndege hiyo ilidunguliwa na walinzi wa anga katika mkoa wa Tver, kaskazini mwa Moscow.

“Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ajali hiyo ya ndege, ambayo imetokea usiku kwenye mji wa Tver.

Maafisa wa huduma za dharura wamesema miili nane imepatikana katika eneo la ajali.

Kumekuwa na maswali mengi mahali aliko Prigozhin tangu alipoongoza uasi huo, lakini hivi karibuni mkanda wa video ilimuonyesha kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram akiwa barani Afrika.  Hiyo ikiwa ni video yake ya kwanza tangu ulipofanyika uasi.

Bosi huyo wa mamluki mwenye umri wa miaka 62 aliongoza uasi tarehe 23-24 Juni, akiwahamisha wanajeshi wake kutoka Ukraine, na kuuteka mji wa kusini mwa Urusi wa Rostov huko Don, na kutishia kuandamana kuelekea Moscow.

Hatua hiyo ilikuja baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya makamanda wa jeshi la Urusi kuhusu mzozo wa Ukraine.

Mgogoro huo ulitatuliwa kwa makubaliano ambayo yaliruhusu wanajeshi wa Wagner kuhamia Belarusi, au kujiunga na jeshi la Urusi.

Prigozhin mwenyewe alikubali kuhamia Belarusi lakini ameweza kusafiri kwa uhuru, akionekana nchini Urusi na pia inasemekana kutembelea Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

error: Content is protected !!