Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Ngorongoro aachiwa, asema harudi nyuma, ashangaa kukamatwa bila kibali cha Spika
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Ngorongoro aachiwa, asema harudi nyuma, ashangaa kukamatwa bila kibali cha Spika

Spread the love

HATIMAYE Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangai (CCM) ambaye alidaiwa kushikiliwa na polisi tangu tarehe 21 Agosti 2023 ameachiwa huru leo huku akisisitiza kwa kuwa yupo upande wa wananchi lazima apate matatizo, na hilo halitomrudisha nyuma hata siku moja. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbunge huyo alidaiwa kushikiliwa na jeshi hilo, akiwa njiani kuelekea kituo cha Polisi wilayani Karatu, kutokana na tuhuma za kuhusishwa kupanga tukio la kushambuliwa waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23 Agosti 2023 Mbunge huyo amesema  amesita kutaja tuhuma alizokutwa nazo na kufafanua kuwa zitajulikana mahakama.

Bila kutaja lini atafikishwa mahakamani, Mbunge huyo wa CCM amedai kwa siku zote tatu alizokuwa ameshikiliwa na polisi hakula chochote.

“Pia nimejifunza kuwa binadamu unaweza kukaa siku tatu bila kula na hautakufa na hata ningekaa siku saba nisingekula siku saba,” amesema.

Aidha, ameeleza kushangazwa na hatua ya polisi kumkamata bila kibali cha Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

“Ninachoshangaa wote wanajua, polisi ndio wanasimamia sheria zetu na Bunge ndio linatunga sheria niliamini kwamba kama walikuwa wananihitaji na hicho ndio nilikuwa nasubiri wangemuandikia Spika barua alafu Spika anijulishe.

“Nakumbuka mwaka jana Aprili niliitwa kuhojiwa kuhusiana na suala la Loliondo, Spika ndio alitoa kibali cha mimi kuhojiwa nashangaa leo kwanini hawakusubiri mpaka Spika atoe barua… najua kuna presha za kisiasa na mimi ni mwanasiasa nitaendelea kuishi kwenye siasa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi wajue yeye ni kiongozi wao hata akikamatwa mara 10 ataendelea kuwa na msimamo wao kwa sababu walimchagua kwa ajili yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!