Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Shule ya msingi yajengwa miaka 25 bila kukamilika, wanakijiji wachoka kuchangia
ElimuMakala & UchambuziTangulizi

Shule ya msingi yajengwa miaka 25 bila kukamilika, wanakijiji wachoka kuchangia

Spread the love

 

Wakazi wa Kijiji cha Makomba kilichopo kata ya Makazi katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora wameililia serikali kwa kuwatenga katika miradi ya maendeleo huku wakichangia gharama zote za ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii ikiwemp elimu, bila msaada wa serikali. Anaandika Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea). 

Wakizungumza na MwanaHalisi Online kutoka kijijini hapo, baadhi wa wakazi hao wamedai kuwa moja ya kero kubwa ya Kijiji hicho ni ujenzi wa shule ya msingi uliogharimu takribani miaka 25 bila kukamilika kutokana na kukosa msaada wa serikali.

Mzee Masanja Philipo anabainisha kuwa kwa miaka mingi ujenzi wa shule hiyo umekuwa ukigharimiwa na wanakijiji wenyewe kupitia michango ya fedha taslimu pamoja na kujitolea kujenga.

Masanja alisema takribani kila mwaka wakazi wa Kijiji hicho wamekuwa wakitoa michango ya kati ya sh 10,000 na 30,000 kwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi katika kaya kwa ajili ya ujenzi huo Pamoja na mchango kupitia mfuko wa jeshi la ulinzi shirikishi (sungusungu) wa Kijiji hicho.

“Tumechoka na michango… tunaomba viongozi wa juu watusikie na waje kutuona nasisi, tunaumia sana kuona wenzetu wilaya jirani hapa ya Kaliua wamejengewa shule, zahanati na barabara za kutosha kila mahali ikiwemo huduma ya umeme huku sisi hapa hakuna hata kimoja kilichofanikiwa” alisema Masanja.

Aliongeza kuwa hata mioundombinu ya barabara, umeme na zahanati haipo katika Kijiji hicho huku maeneo jirani yaliyopo upande wa wilaya ya Kaliua yakiwa yanaendelea kuboreshwa na serikali.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mnyeshi Ng’ombengeni alithibitisha kuwa ujenzi wa miundombinu ya elimu, barabara na zahanati umekosa msaada wa serikali kwa muda mrefu jambo ambalo liliwafanya wakazi kuanzisha ujenzi wa shule na kuendelea kujenga kupitia michango ya wananchi pekee.

“Serikali imetusahau, kijiji hiki kwani hakuna msaada wowote tuliowahi kuupata katika ujenzi wa miundombinu, hadi sasa, Kijiji cha Makomba hatuna barabara yoyote, hivyo tunalaziomika kwenda kulala Kijiji cha Sawewe ili tupate magari ikiwa tunataka kwenda mjini kufuata mahitaji na kuhusu shule… hatujawahi kupata msaada wowote kutoka serikalini tumekuwa tukichangishana na wakazi tu hapa hadi tumekamilisha ujenzi wa madarasa manne na nyumba moja ya walimu ambayo yote yanatumika lakini hayajakamilika ipasavyo,” alisema Mawenyekiti wa Kijiji hicho.

Aliongeza kuwa hata sasa kuna mchango unaendelea ili kuendeleza ujenzi wa jengo la madarasa linaloendelea shuleni hapo pamoja na jengo la zahanati ambalo limefikia kiwango cha lenta kwa nguvu ya wananchi wenyewe bila msaada kutoka serikalini.

“Kwa mwaka huu, tunaendelea na mchango wa Sh 15,000, kwa kila mtu mwenye umri wa kufanya kazi. Michango hii ni mzigo mkubwa kwani hatutakamilisha hata ujenzi wetu na hali ni ngumu sana ni kama kianzio mwaka jana tulichangia Sh10,000 kila mtu, kutoka mfuko wa sungusungu tukachangia milioni tisa, lakini hatujakamilisha ujenzi wetu” amesema Mwenyekiti Mnyeshi.

Paskali Joseph, mkazi wa kikiji hicho alisema kuwa, Viongozi wa serikali hawajawahi kufika tangu kuanzishwa kwa Kijiji hicho, isipokuwa viongozi wa vyama vya siasa na wagombea tu ambao huonekana nyakati za kampeni na kupotea jumla mara baada ya kushinda ama kushindwa uchaguzi.

“Kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 mgombea wa ubunge, Almas Maige alileta bandari 10 za mabati ambayo yaliweza kuezeka madarasa mawili na baada ya kushinda uchaguzi alipotea jumla hadi leo hajawahi kukanyaga hapa” alieleza kwa masikitiko makubwa Mzee huyo na kuongeza kuwa ujenzi wa shule hiyo ulianza tangu mwaka 1997 kabla ya majengo hayo kuangiuka na kuanzishwa tena baada ya miaka kadhaa 2005.

Mzee Paskali alisema kuwa Wanamakomba, mambo ya ujenzi wa madarasa na huduma zingine muhimu wanayasikia katika vyombo vya habari tu wao hawaoni chochote wala kiongozi wa serikali kufioka kuona hata juhudi zao wenyewe wanazozifanya katika kujenga miundombinu ya huduma za elimu, afya na barabara.

“Kijiji hiki tumetengwa kama kisiwa ambacho viongozi hawatutambui kabisa kwani hata kuisajiri shule hii tulipata shida sana hadi tulipofanikiwa kuongea na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora alipokuja kunadi wagombea wa Ubungen a Udiwani katika kampeni za Uchaguzi ndipo shule ikasajiriwa” Aliongeza Mzee Paskali. .

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wakazi maskini wa kijijini hicho ambao ni walengwa wa mfuko wa kunusuru kaya maskini wa TASAF wamekuwa wakishiriki kuchimba barabara kwa majembe ya mkono kama sehemu ya jukumu la wanufaika wa TASAF kijijini hapo ili waweze kupewa fedha hizo.

Akizungumzia suala hilo, msimamizi wa TASAF kutoka kijijini hapo, Sayi Ngelela alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa mradi wa walengwa wa TASAF kushirikia ujenzi wa barabara inayounganisha Kijiji cha Makomba na Kijiji Jirani chs Sawewe kwa kutumia majembe ya mkono, hali imekuwa ngumu sana kiasi cha kupelekea baadhi ya walengwa wa TASAF wakiwemo kinamama kujitoa katika mradi huo kwa madai kuwa kazi hiyo ni ngumu na bado pesa hizo hawazipati kwa wakati.

“Niliajiriwa kama msimamizi wa mradi huu na tangu tuanze ni miezi miatatu sasa lakini bado sijawahi kulipwa hata pesa ya mwezi mmoja japo nilisaini mkataba wa kulipwa laki tatu kwa mwezi kama Msimizi wa mradi huo hapa kijijini” alieleza msimamizi huyo ambaye ni kijana mwenye umri wa miaka 26 na kuongeza kuwa kusuasua kwa ujio wa fedha hizo umepelekea kupungua kwa washiriki wa uchimbaji wa barabara hiyo kwani wanapungua kila siku na hadi sasa wamebaki watu 40 wanaojitokeza.

Baadhi ya wanufaika wa mradi huo walieleza kuwa, awali wakati wakisajiliwa walielezwa kuwa serikali inawasaidia wazee maskini kujikimu lakini baadaye wameingizwa katika mpango wa kuchimba barabara ndipo kwa majembe ya mkono hali inayowaumiza kwani mtu asposhiriki anakatiwa sehemu yake ya kuchimba hadi siku atakapokuja.

“Walipokuja kusajili maofisa wa TASAF walisema serikali inasaidia wazee na maskini kujikimu kiuchumi lakini tumeshangaa kuona hadi wachimbe barabara kwa mikono wakati huohuo fedha haina mpangilio mzuri. Mara ije kila mwezi, ama miezi mingi inapita bila kuletewa fedha hizo, wakati mwingine inakuja nyingi mara pungufu huku tukiambiwa imekatwa kidogo kwa ajili ya posho ya afisa aliyeileta jambo Iinalotuchanganya,” alieleza Masanja Philipo na kuomba serikali iingilie kati ili kuwasaidia wananchi hao.

Wakazi hao pia walieleza kuwa Kijiji cha Makomba hakina hata ofisi ya Kijiji, viongozi wamekuwa wakifanya vikao chini ya mwembe baada ya ofisi iliyojengwa kwa mfuko wa Sungusungu kubomoka ukuta.

“Hata ofisi kijiji chetu haina, nyaraka za serikali zipo nyumbani mwa mtu, anaishi nazo mwenyekiti wa kijiji na wakati mwingine inawezekana viongozi kuwa wanaendesha mashauri nyumbani kwao tangu jingo letu tulilojenga kwa mfuko wa Sungusungu mwaka 2019 lilipobomoka , hali iliyopelekea serikali kuanza kuendesha shughuli zake chini ya mwembe hapa senta” alisema Paskali Joseph huku akiomba serikali itsaidie kukamilisha ujenzi wa miundombinu za mawasiliano, zahanati, umeme, barabara na shule kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Jirani akitolea mfano vijiji Jirani vya wilaya ya Kaliwa.

Mpaka sasa wanakijiji hao wamefanikiwa kujenga madarasa manne yanayotumika lakini yote hayajasakafiwa na wameongeza banda la nyasi ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi huku ujenzi wa jingo jingine lenye madarasa mawili ukifikia hatua ya renta, yote hay ani kwa juhudi za wananchi wenyewe bila msaada wowote bkutoka serikalini.

Shule hiyo inaarifiwa kuwa inawalimi sita kwasasa ambao kati yao mwalimu mmoja ni wakike, ina choo chenye mashimo nane kwa ajili ya wanafunzi huku walimu wote wakidaiwa kuwa na choo chenye shimo moja.

Katika kuwezesha makazi ya walimu hao, Wanakijiji wamekamilisha ujenzi wa nyumba ya walimu yenye vyumba vitatu na sebule moja kwa kujitolea mahitaji yote kwa michango ya wanakijiji na sungusungu Pamoja na kujitolea kufanya kazi kwa zamu katika shughuli za ujenzi.

Hata hivyo, kuna uhitaji mkubwa wa nyumba za walimu, kwani mpaka sasa shule ya Makomba inawalimu sita huku nyumba iliyopo wanaishi walimu watatu na wengine wakiishi katika maeneo yao nje ya shule hiyo.

Pamoja na changamoto zilizopo, shule hiyo inaripotiwa kuwa na matokeo mazuri kwani katika matokeo yake ya kwanza kwa wahitimu wa darasa la saba mwaka 2021, ni wanafunzi wawili tu waliofeli mtihani huku wengine wote wakifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari na kwa mwaka 2022, katika matokeo ya darasa la saba ni mwanafunzi mmoja aliyefeli mtihani, hali iliyofanya shule hiyo kushika nafasi ya saba ki-wilaya ya Uyui na nafasi ya 99 kimkoa wa Tabora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!