MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA), Profesa Shadrack Mwakalila amewataka wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo kwa mwaka 2022/20223 kuzingatia zaidi masomo ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii, juhudi na maarifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Aidha, Profesa Mwakalila amewataka wanafunzi hao kuwa waadilifu, waaminifu na kuzingatia suala la ulipaji ada kwa wakati.
“Suala la kulipa ada ni la muhimu sana, kabla ya kuja hapa chuoni kila mmoja alijipanga kuja kusoma, hili siyo jambo la dharura na ilikuwa ni mipango ya muda mrefu hivyo ni wajibu ada ilipwe kwa wakati,” alisistiza Profesa Mwakalila.
Mkuu huyo wa Chuo amewataka pia wanafunzi hao kujiepusha na udanganyifu wa aina yoyote pindi wanapokuwa chuoni.
Pia amewataka kujiepusha na mambo ambayo hayawezi kumsaidia katika masomo, na migogoro yoyote au makundi ya uchochezi na suala zima la kuheshimiana kati ya walimu na wanafunzi.
Leave a comment