
MPANGO wa “Shule Direct” yenye kauli mbiu “jifunze mahali popote, wakati wote” inayomwezesha mwanafunzi kutumia simu ya mkononi au kompyuta kujifunza imetajwa kuchochea kiwango cha wanafunzi kuongeza uelewa wa masomo, anaandika Pendo Omary.
Mwaka 2013 ulianzishwa mpango ambao unalenga kuwahudumia wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha nne wa shule za sekondari.
Iku Lazaro, Ofisa habari wa Direct Shule akizungumza wakati wa warsha ya kushirikishana uzoefu na mikakati ya elimu mbadala kwa wasichana, amesema mfumo huu unamuwezesha pia mwanafunzi kutunga maswali.”
“Kupitia program hii mwanafunzi anaweza kupata masomo 11-. anaweza kuuliza maswali na kuna jopo la walimu watakaomsaidia majibu. tayari kupitia program hii wanafunzi milioni moja wamefikiwa, walimu 15397 wanatumia mtandao huu kuelekeza wanafunzi,” amesema Lazaro
More Stories
Shule ya Kandwi Z’bar yapata neema
Wanafunzi walilia madarasa Mtwara, Silinde awajibu
Shule yenye darasa moja tangu 2014