Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Wanaharakati wamkumbusha Rais Magufuli milioni 50
Habari Mchanganyiko

Wanaharakati wamkumbusha Rais Magufuli milioni 50

Spread the love

WANAHARAKATI wa maendeleo haki za binadamu na usawa wa kijinsia wameitaka Serikali kutekeleza ahadi yake ya kutoa Sh. 50 milioni kwa kila kijiji ili kuharakisha maendeleo katika vijiji, anaandika Pendo Omary.

Rai hiyo imetolewa leo katika tamasha la jinsia la 14 linaloendelea katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), ambapo mada kuu ni “mageuzi ya mifumo kandamizi kwa usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu.”

Ahadi hiyo ya kutoa fedha hizo ilitolewa na Rais John Magufuli wakati akiwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Imeelezwa kuwa utekelezaji huo utasaidia kuhamasisha maendeleo katika vijiji wakati ambapo halmashauri nyingi zimeshidwa kutekeleza maamuzi ya serikali ya kila halmashauri kutenda asilimia 10 ya mapato yake kuelekeza kwa wanawake na vijana katika kuwainua kiuchumi.

Tatu Maleta, Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Jitambue cha Kisaki amesema kama “serikali itatimiza ahadi yake, wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini watajikwamua kiuchumi, kwa kutumia fedha hizo katika kufanya biashara.”

Aidha, Maleta ambaye pia ni Ofisa Habari wa Jukwaa la Wakulima Wadogo Kanda ya Pwani, ameitaka serikali kuongeza fedha za ruzuku zinazotolewa kwa ajili ya wakulima wanawake ambazo zimepungua kutoka asilimia 10 hadi 4.6.

“Kitendo cha serikali kupunguza fedha hizo za ruzuku, kimeleta athari kwa wakulima wadogowadogo. Kilimo ndio uti wa mgongo, awali ilivyokuwa asilimia 10 ilikuwa haitoshi na sasa imepunguzwa ndio haitoshi kabisa, na wanawake ndio waathirikaji kwa kuwa ni wazalishaji wakuu na wachangiaji wa pato la taifa,” amesema Maleta.

Changamoto nyingine zinazorudisha nyuma maendeleo ya wanawake wanaojishughulisha na kilimo ni; uhaba wa pembejeo, miundombinu mibovu maeneo ya vijijini hasa barabara, kukosekana kwa masoko ya uhakika ya bidhaa pamoja na kuuza mazao yao kwa bei ya hasara.

Kwa upande wake Fatma Abdulrahman, mshiriki wa tamasha hilo amesema changamoto nyingine inayowakwamisha wakulima wadogo ni kukosa mikopo kutoka katika taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Kilimo kutokana na kuwekewa masharti magumu ikiwemo riba kubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

error: Content is protected !!