Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shaka: Rais Samia hana ‘mbambamba’ kwenye maendeleo
Habari za Siasa

Shaka: Rais Samia hana ‘mbambamba’ kwenye maendeleo

Katibu wa Itikadi na uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka
Spread the love

 

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hana masihara na jambo linalobusu maendeleo ya wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Amesema katika kuthibitisha hilo, katika kipindi chake kifupi ameweka histori ya kuwa kiongozi wa kwanza kufikisha umeme wa gridi mkoani Kigoma jambo ambalo halikuwa limefanyika katika kipindi cha zaidi ya miaka 60 ya uhuru nchi.

Shaka ameyasema hayo jana Oktoba 17, 2022, mjini Kasulu mkoani Kigoma, baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimia wananchi akiwa katika msafara wa Rais Samia ambaye yuko ziarani mkoani humo.

“Ndugu Mwenyekiti (Rais Samia) ukitaka kujua raha angalia wana Kasulu leo wanavyoonesha mbwembwe, eti wanawasha taa mchana…baada ya miaka 60 ya uhuru wa nchi hii Rais Samia amefanya maajabu makubwa, Rais Samia hana ‘mbambamba’ katika kuleta maendeleo ya Watanzania,” amesema.

Amesema kinachofanywa na Ras Samia na serikali yake ni kutekeleza ahadi ya CCM ya kuwaletea maendeleo wananchi.

“Dawa ya deni ni kulipa, CCM ilichukua dhamana ya deni kwa Watanzania na wana Kasulu na wana Kigoma mwaka 2020. Ndugu Mwenyekiti kwa hali tuliyoiona leo tumeshuhudia namna ambavyo mkilipa deni hili kupitia Ibara ya 80 pale ulipokwenda ukaweka jiwe la msingi la kuzindua shule ya kisasa.

“Lakini tumeshuhudia namna ambavyo mnalipa deni hili kupitia uimarishaji na uboreshaji wa nishati ya umeme, Ibara ya 63 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM inavyotekelezwa kwa ufanisi mkubwa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

error: Content is protected !!