Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serukamba aanika mafanikio ya Singida
Habari za Siasa

Serukamba aanika mafanikio ya Singida

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amesema tangu Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan iingie madarakani, bajeti ya mkoa huo imeongezeka kwa asilimia 327.6 hadi kufikia Sh. 530 billioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida…(endelea).

Serukamba ametoa taarifa hiyo akizungumzia ziara ya Rais Samia mkoani Singida, inayoanza leo tarehe 15 Oktoba 2023.

“Tunashukuru sana tumepata ugenzi wa Rais Samia na wananchi wamempokea kwa furaha kutokana na kazi kubwa aliyofanya katika mkoa Wetu. Ameongeza bajeti yetu hususan fedha za miradi ya maendeleo,” amesema Serukamba.

Serukamba amesema kuwa, Rais Samia anatekeleza kwa vitendo maono ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ya kupambana na maadui watatu wa taifa, umasikini, maradhi na ujinga, kwa kuongeza fedha za miradi ya maendeleo kwenye sekta za afya, kilimo na elimu.

Amesema mkoani humo, Serikali ya Rais Samia imejenga hospitali nne za wilaya, vituo vya afya 22 na zahanati 69.

Kwenye miradi ya elimu, Serukamba amesema Serikali ya Rais Samia inaendelea kujenga Shule za sekondari mkoani humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

error: Content is protected !!