Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yawatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa mafuta
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yawatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa mafuta

Spread the love

Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema kuwa hali ya utoshelevu wa mafuta nchini kwa kipindi cha  mwezi Julai hadi Septemba ni ya kuridhisha na  Serikali kupitia Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa  Pamoja (PBPA) inaendelea kuingiza mafuta kwa mujibu wa taratibu na mikataba iliyowekwa na kukubalika.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Dk. Biteko amesema hayo leo tarehe 19 Oktoba 2023 jijini Dodoma wakati Wizara ya Nishati ilipokuwa ikitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu hali ya uagizaji wa mafuta nchini pamoja na upatikanaji wa fedha za kigeni


“Ujazo wa mafuta yaliyokuwepo nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani mwishoni mwa mwezi Septemba, 2023 yalikuwa ni jumla ya lita 248,815,232 ikiwa ni lita 136, 532,747 za dizeli, lita  93,305, 815 za petroli na lita 18,978, 670 za mafuta ya ndege na taa” amesema.

Aidha, amesema kuwa, bakaa hiyo ya mafuta inajumuisha mafuta yaliyokuwepo katika maghala ya mafuta na yale yaliyokuwa katika hatua za upakuaji na wastani kila wakati kumekuwa na ziada ya mafuta isiyopungua siku 15 kwa dizeli na petroli wakati ambapo kwa mafuta ya ndege ziada huzidi siku 30.

Kuhusu suala la upatikanaji wa Fedha za kigeni nchini,  Waziri wa Fedha, Dk.  Mwigulu Nchemba amesema sababu za uhaba wa fedha za kigeni umechangiwa na athari za uviko-19, kwa kusababisha ukuaji wa uchumi wa mataifa mbalimbali duniani.

Amesema uchumi wa Tanzania ulikuwa kwa takriban asilimia 4.9 , mdororo wa kiuchuni uliosababishwa na kufungwa kwa baadhi ya shughuli za uchumi kama vile China, na athari za vita ya Ukraine na Urusi  na hivyo kusababisha ongezeko la bei katika soko la dunia.

“Pia mabadiliko ya tabia ya nchi na ongezeko la riba nchini Marekani vimechangia na hivyo kusababisha mahitaji makubwa ya fedha ya kigeni hususani Dola za Marekani,” amesema.

Amesema, Tanzania imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na upungufu huo ikiwa ni pamoja na kuziagiza Wizara kuunda timu ya wataalamu kufanya upembuzi wa kina kuhusu  changamoto hiyo na kuziagiza taasisi kufanya uchambuzi wa maeneo mengine yenye matumizi makubwa ya fedha za kigeni.

Kwa upande wake,  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba akitoa majumuisho kwa kamati amesema kuwa miongoni mwa hatua ambazo zimechukuliwa kwa ajili ya kuboresha hali ya upatikanaji wa mafuta ni pamoja na kuanza kutumia eneo la  kushushia mafuta  la TIPER ili kupunguza muda wa kushusha mafuta.

Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kupitia kwa Mwenyekiyi wake. Daniel Sillo wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa mafuta nchini kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2023 hadi sasa na kuwatoa hofu wananchi kuhusu kukosekana kwa  bidhaa hiyo nchini na kueleza kuwa hatua zilizochukuliwa na Serikali zinaridhisha.

Kikao cha Kamati ya Bunge ya Bajeti kilihudhuriwa pia na wakuu wa taasisi kutoka EWURA, PBPA, BOT na wadau mbalimbali kutoka Sekta ya Mafuta na Fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!