Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yashusha neema Njombe
Afya

Serikali yashusha neema Njombe

Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeshusha neema kwa wananchi wa Njombe kwa kutenga kiasi cha Sh. 7.6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ili kuboresha huduma kwa Wananchi. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea). 

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya amezungumza hayo katika zoezi la uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Katika uzinduzi huo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya katika Mkoa wa Njombe ikiwemo kujenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, jengo la maabara, jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, wodi za wagonjwa gorofa tatu, nyumba za Watumishi tano, pamoja na kichomea taka.

“Tunajenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, tunajenga jengo la jengo la maabara, tunajenga jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji ghorofa mbili, tunajenga wodi za wagonjwa ghorofa tatu, tunajenga jengo la kufulia, tunajenga kichomea taka na tunajenga nyumba za watumishi tano,” amesema.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa Hospitali hiyo kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa majengo hayo hayo ndani ya miezi kumi ili wananchi waanze kufaidika na huduma za Afya katika Hospitali hiyo, huku akiwatoa hofu kuwa pesa zote zipo tayari.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amewaasa Wananchi kupambana dhidi ya magonjwa yasiyo yakuambukiza kama kisukari, shinikizo la damu, saratani na magonjwa ya moyo kwa kubadilisha mtindo wa maisha ikiwamo ulaji ulio sahihi, kuacha uvutaji wa sigara na tumbaku, kuacha unywaji wa pombe kupita kiasi pamoja na kutofanya mazoezi mara kwa mara.

Aidha, ametoa wito kwa vijana kujiepusha na mambo ambayo yatapelekea kupata maambukizi ya VVU, huku akiweka wazi kuwa maambukizi mapya ya VVU ni 82,000 kila mwaka nchini Tanzania, huku katika kila watu 100, watu 40 ni vijana wenye umri kati ya 15 hadi 24 umri ambao ni nguvu kazi ya taifa.

“Tunatambua kwamba kuna maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi Mkoani Njombe, lazima tuzingatie kanuni za kujikinga na maambukizi ya VVU, kujizuia kufanya mapenzi kwa vijana hasa kwa wasichana ambao muda wao haijafika, pili kuwa mwaminifu kwa mwenza wako au mpenzi wako na tatu kutumia kinga,” alisema Waziri Ummy.

Christopher Olesendeka, Mkuu wa mkoa wa Njombe amewatoa hofu wananchi wa mkoa huo kwa kuweka wazi kuwa huduma za Afya katika Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa haitoathiri utoaji huduma katika Hospitali ya Kibena iliyokuwa Hospitali ya Mkoa, ambayo kwa sasa imerudishwa chini ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.

“Nitahakikisha wale Watumishi ambao tulikubaliana waje kwenye Hospitali hii, waje na nguo zao, vifaa vyote waviache Kibena na huduma ya Kibena iendelee, na kazi ya Hospitali hii Waziri  na Rais wataweka vifaa vyote vitakavyohitajika na huduma zitaendelea,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!