Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaahidi ajira zaidi sekta ya usafirishaji
Habari Mchanganyiko

Serikali yaahidi ajira zaidi sekta ya usafirishaji

Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete akimtunuku Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Lojistiki na Usafirishaji Farida Salum katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Spread the love

Serikali imewahakikishia wahitimu wa kozi mbalimbali za usafirishaji kuwa itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya usafiri na usafirishaji pamoja na kuzingatia ongezeko la wataalam ili kuhakikisha miundombinu inasimamiwa kwa kuzingatia weledi. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Akizungumza katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Nchini (NIT) jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete amesema soko la ajira katika sekta ya usafirishaji limeongezeka kutokana na maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali kwenye bandari, ujenzi wa meli, viwanja vya ndege, na ununuzi wa ndege.

“Sekta ya usafiri na usafirishaji inakuwa kila siku na uwekezaji unaendelea kufanywa kwenye miundombinu, nyinyi kama wahitimu mtaweza kupata ajira kwenye maeneo ya reli, bandari na viwanja vya ndege kupitia uwekezaji huu”, amesema.

Naibu Waziri Mwakibete ametumia fursa hiyo kuwaasa wahitimu kuzingatia misingi ya uadilifu waliyofundishwa kwani usimamizi wa miundombinu unahitaji nidhamu na uadilifu ili kuifanya iweze kudumu kwa muda mrefu.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete ameipongeza NIT kwa kuhakikisha inaongeza kozi katika njia tano za usafirishaji na kupunguza gharama kubwa inayotumia Serikali kwa kuwasomesha wataalam wa fani hizo nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zacharia Mganilwa amesema kwa sasa chuo kimeongeza udahili na kufikisha wanafunzi zaidi ya elfu kumi na mbili kwa mwaka 2022 ikilinganishwa na wanafunzi elfu sita kwa mwaka 2020.

Profesa Mganilwa ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kununua ndege mbili zenye injini moja kwa ajili ya shule ya usafiri wa anga zitakazosaidia wanafunzi wa urubani na uhandisi wa ndege.

Katika Mahafali hayo ya 38, wanafunzi zaidi ya 2700 wametunukiwa shahada za uzamili, shahada, stashahada za juu, shahada na astashahada katika maeneo mbalimbali ya Usafirishaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

error: Content is protected !!