TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia (Costech) imetoa Sh milioni 50 kwa wabunifu wa wanawake watano walioshinda shindano la Buni Divaz. Anaripoti Faki Sosi … (endelea)
Shindano hilo lililowashindanisha wabunifu wanawake 35, watano kati yao waliokuwa na mawazo bora wameshinda.
Buni Divaz ni shindano lililoandaliwa na Costech kupitia kitengo cha ubunifu.
Akizungumza katika utoaji wa zawadi hizo Mkurugenzi wa tume hiyo Dk. Amos Nungu amesema mashindano hayo yemelenga kuwainua wabunifu wanawake na kuondosha fikra ya kwamba masuala ya teknolojia na Sayansi ni ya wanaume pekee.
Amesema nafasi hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya wabunifu wanawake ili kuwaongezea ari wanawake kwenye ulimwengu wa ubunifu hasa wa teknolojia.
“Tumeona maeneo mengi wabunifu ni wanaume ndio wameshika hatamu, Tume tumetoa nafasi hii maalum kwa wanawake ili waonyeshe mawazo yao” amesema.
Amesema kuwa Tume hiyo haitaishia kutoa fedha tu, bali itaendelea kuwalea wabunifu hao mpaka wanafikia malengo yao.
Christina Charles Mwanzilishi wa Bionutrion Company, alisema wazo lake ni miongoni mwa mawazo bora yaliyomfanya kuibuka mshindi.
Amesema ushindi huo umemtia moyo na hamasa kwa wanawake wengine waone umuhimu wa kushiriki masuala ya teknolojia.
Leave a comment