Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wenyeviti CHADEMA waungana na Mbowe kuanza mikutano Januari
Habari za Siasa

Wenyeviti CHADEMA waungana na Mbowe kuanza mikutano Januari

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

WAKATI kukiwa na hofu kuwa kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kwamba ataendelea na mazungumzo ya maridhiano imekigawa chama hicho, wenyeviti wa mikoa wameibuka na kumuunga mkono kiongozi wao.

Aidha, wenyeviti hao wamesema wanajiandaa kwa mikutano ya ndani na hadhara kuanzia mwakani kama Katibu wao John Mnyika alivyoagiza. Anaripoti Selemani Msuya…(endelea).

Msimamo wa wenyeviti hao umetolewa na wenyeviti watatu kwa niaba ya wenzao wakati wakizungumza na waandishi wa habari jana  tarehe 18 Disemba, 2022 jijini Dar es Salaam.

Wenyeviti waliotoa msimamo huo William Mungai wa Iringa, Henry Kileo Kinondoni na Emmanueli Ntobi wa Shinyanga.

Akizungumzia uamuzi wa wenyeviti hao kuungana na Mwenyekiti Mbowe, Mungai amesema maridhiano ni njia muhimu katika kuwezesha nchi na wananchi kupata maendeleo.

Mungai amesema CHADEMA ni chama ambacho kinaamini katika maridhiano, hasa katika kipindi hiki ambacho Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia hiyo.

Amesema maridhiano sio kwamba yananufaisha CHADEMA bali ni wananchi hivyo wanaendelea kuungana na Mwenyekiti Mbowe na wenzake ambao wapo katika mazungumzo.

“Sisi tunataka nchi hii, kila mtu aweze kufaika na matunda yaliyopo, ndio maana tunaungana na viongozi wetu waliopo kwenye mazungumzo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), tutatangaza kutounga mkono iwapo viongozi wetu watasema wameshindwa,” amesema.

Mungai amesema iwapo Watanzania waishi kwa upendo, umoja na amani maendeleo yatapatikana kwa kasi kubwa, hivyo wamewataka wana CHADEMA kuungana na viongozi wao katika mchakato huo wa maridhiano

Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Iringa amesema kupitia mazungumzo ya maridhiano wanaamini Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba mpya vitapatikana.

“Wanachadema waendelee kujipanga kujenga chama chao bila woga kwani viongozi wetu wanania njema,”amesema.

Akizungumzia maagizo ya Katibu Mkuu Mnyika kwa mikoa kuanza opereseheni ya ujenzi wa chama, Mwenyekiti wa Mkoa wa Kinondoni Kileo amesema wamejipanga kutekeleza maelekezo hayo bila kikwazo chochote.

Amesema wao kama wabunge na wenyeviti wa CHADEMA mkoa watahakikisha wanajenga chama kama Katiba inavyotaka na kwamba kutokufanya mikutano labda Rais atangaze kuwa kuna hatari.

Kileo amesema hawapo tayari kuona mtu yoyote anakwamisha mikutano hiyo, hivyo wanasisitiza kuwa kuanzia Januari mwakani wataanza opereseheni ya CHADEMA digital na mikutano ya hadhara.

“Sisi wenyeviti tumejipanga kutekeleza maagizo ya chama kwa asilimia 100 asitokee mtu yoyote kuzuia, hatutakubali, labda Rais Samia atangaza kuna hatari,” amesema.

Kwa upande mwingine Kileo amewataka wana CHADEMA kupuuza watu ambao wanapotosha kuhusu mazungumzo ya maridhiano ambayo yanayoendelea kati ya chama chao na CCM.

Mwenyekiti huyo amesisitiza umuhimu wa wanachama wao kusimamia hoja zao za msingi na wasikubali kupelekwa na upepo ambao una lengo la kuwaharibia mipango yao.

Naye Mwenyekiti Ntobi wa Shinyanga amesema wanachosimamia viongozi wao kuhusu maridhiano ni maelekezo ya chama hivyo hakuna mtu ambaye amelambishwa asali kama inavyodaiwa.

Amesema wamejipanga kusimamia maslahi ya chama kwa nguvu zote na kwa hapo tayari kuungana na upotoshaji wowote.

“Sisi kama chama hatujawahi kukaa na kupanga kujitoa kwenye maridhiano, ila ninachojua tulikubaliana kuingia kwenye maridhiano na tunaahidi kuunga mkono hadi hapo ambapo itataarifiwa kivingine,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!