Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali ya Tanzania yafikishwa mahakamani
Habari za Siasa

Serikali ya Tanzania yafikishwa mahakamani

Kajubi Mkajanga, Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Spread the love

 

ASASI za kiraia nchini Tanzania, zimeifikisha katika Mahakama ya Afrika Mashariki serikali ya nchi hiyo kwa kukiuka amri halali ya Mahakama. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo … (endelea).

Kesi hiyo imefunguliwa jana Ijumaa tarehe 28 Agosti 2021, Mahakama ya Afrika Mashariki na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Kesi hiyo namba 37 ya mwaka 2021, imefunguliwa dhidi ya Serikali ya Tanzania, baada ya kukiuka amri halali ya Mahakama kwa kutumia vifungu vya Sheria ya Huduma ya Habari namba 12 ya mwaka 2016 vilivyobatilishwa na Mahakama ya Afrika Mashariki.

MCT, LHRC na THRDC walifungua kesi hiyo wakipinga vipengele mbalimbali vya sheria ya hudumu ya habari kuwa vilikuwa vinakiuka mkataba wa Africa Mashariki na vilikuwa kinyume na misimgi ya haki za binadamu na utawala.

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu Taifa

Tarehe 11 Aprili 2019, Serikali ilionesha nia ya kukata rufaa lakini haikukata rufaa na nia hiyo ilifutwa na Mahakama ya kitengo hicho cha rufaa tarehe 9 June 2020.

Mkurugenzi wa Habari Maelezo alisimamisha gazeti la Uhuru tarehe 11 Agosti 2021 kwa siku 14 , akitumia kifungu cha 9(b) kwa kwenda kinyume na vipengele vya 50 na 52 vya sheria ya huduma ya Habari.

Gazeti hilo, lilifungiwa baada ya kuandika habari ya upotoshaji kuhusu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba hatogombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2025.

Vifungu 50 na 52 vya sheria vilitumiwa na mkurugenzi vilibatilishwa na Mahakama ni kudharau amri halali ya Mahakama kwa makusudi.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Tarehe 28 Machi 2019, hukumu ilitolewa na mahakama kubatilisha vifungu 7(3) (a),(b),(c),(f),(g),(h),(i),(j),19,20 na 21,35,36,37,38,39,40,50,52,52,53,54,58 na 59 vya sheria hiyo baada ya walalamikaji kupeleka maombi lakini mpaka sasa serikali ya Tanzania haijatekeleza amri ya Mahakama.

Shauri hilo limefunguliwa ili kuitaka na kuiomba Mahakama kuchukua hatua kwa ukiukaji uliotokea wa wazi wa sheria na wajibu wa serikali ya Mungano wa Tanzania chini ya Mkataba wa Afrika Mashariki

Ikumbukwe kuwa tarehe 11 January 2017 MCT, LHRC na THRDC walifungua shauri mbele ya Mahakama ya Afrika Mashariki Shauri Na. 2/2017 wakipinga vipengele mbalimbali vya Sheria ya Huduma ya Habari kuwa vilikuwa vinakiuka mkataba wa Afrika Mashariki na vilikuwa kinyume na misingi ya haki za bainadamu na utawala bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!