October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kujenga madarasa 15,000, vituo vya afya 250

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kuna fedha ambayo ameipata na sasa anatarajia kushirikiana na halmashauri zenye uwezo kifedha kujenga madarasa 15,000 nchi nzima licha ya kuwepo kwa uhaba wa madarsa 11,000 hadi sasa. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo … (endelea). 

Pia amesema alipoingia madarakani Machi 19 mwaka huu amekutana tarafa 250 hazina vituo vya afta, hivyo atatumia tozo za miamala ya simu kujenga vituo hivyo katika tarafa zote.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Septemba, 2021 jijini Dodoma wakati akihutubia Mkutano Mkuu maalumu wa uchaguzi wa viongozi wakuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) wenye kauli mbiu “chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu.”

“Sina maana kwamba halmashauri zenye fedha nyingi hiyo fedha itakuwa exempted kwenye kujenga madarasa hapana.

“Ni ile ambayo serikali kuu itatafuta na halmashauri zenye uwezo tutakwenda kushirikiana kujenga mdarasa hayo 15,000. Lengo ikifika 2022 watoto wote waingie shule kwa pamoja,” amesema.

error: Content is protected !!