Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi kina Mbowe: Mshtakiwa apata kigugumizi
Habari za SiasaTangulizi

Kesi kina Mbowe: Mshtakiwa apata kigugumizi

Spread the love

 

ADAM Kasekwa, mshtakiwa wa pili katika kesi ndogo ya kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, amepata kigugumizi kujibu swali aliloulizwa na wakili wa jamhuri, Abdallah Chavula wakati anatoa utetezi wake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu, tarehe 27 Septemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mustapha Siyani, wakati kesi hiyo ndogo inasikilizwa.

Ni baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Adballah Chavula, alipomuuliza mshtakiwa huyo mahakama ichukue kauli ipi kati ya maelezo yake aliyowahi kutoa mahakamani hapo, akidai alitoa maelezo yake ya onyo katika Kituo cha Polisi Mbweni mkoani Dar es Salaam, kwa mateso.

Na maelezo aliyotoa akidai, alichukuliwa maelezo yake baada ya kutishwa na sio kuteswa.

Swali hilo lilimpa kigugumizi Kasekwa kulijibu, akidai wakati aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Arusha, ACP Ramadhan Kingai, anamsainisha karatasi yenye maelezo ya onyo hakumpiga bali alimtesa.

Jibu hilo halikuiridhisha mahakama hiyo, ambapo Jaji Siyani alitoa nafasi nyingine kwa Wakili Chavula, kuuliza swali ili mshtakiwa huyo alielewe kisha alijibu kwa ufasaha.

Wakili Chavula alimhoji tena shahidi huyo kwamba kauli ipi ni sahihi kati ya alikuwa anateswa na alitoa maelezo hayo baada ya kuteswa na ile aliyodai, alipofikishwa Dar es Salaam, hakuteswa bali alipewa karatasi yenye maelezo hayo na kuambiwa asaini na aweke maneno ya uthibitisho.

Kasekwa alijibu akidai, wakati anachukuliwa maelezo ya onyo hakupigwa bali alipata mateso ikiwemo ya kufungwa pingu.

Hata hivyo, Jaji Siyani alimtaka Kasekwa achague ajibu sahihi na kama atakuwa anakosea wakili wake, John Mallya atamsaidia.

Pia, Jaji Siyani alisema majibu ya mshtakiwa huyo katika swali hilo ni muhimu, kwa kuwa mahakama hiyo inayategemea katika kutoa uamuzi.

Wakili Mallya alinyanyuka na kumsaidia mteja wake, akidai mteja wake amejibu akidai hakupigwa na ACP Kingai, lakini hakumaanisha kama hakuteswa kwani hata kufungwa pingu ni mateso pia.

Naye Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alinyanyuka na kusema ili kuondoa mtanziko huo, Wakili Chavula anatakiwa atafute namna bora ya kumuuliza swali shahidi huyo, badala ya kushindana.

Kufuatia kauli hiyo ya Wakili Kibatala, Jaji Siyani alimhoji mshtakiwa huyo mahakama hiyo iandike kama hakupigwa mkoani Dar es Salaam, ambaye alijibu akidai ndiyo Dar es Salaam hakupigwa.

Kasekwa alijibu akidai, alitoa maelezo bila ya mateso lakini alitoa maelezo chini ya mateso.

Shahidi huyo ambaye pia ni mshtakiwa anaendelea kutoa ushahidi wake akihojiwa na Wakili Chavula.

Alianza kutoa ushahidi wake Ijumaa iliyopita, tarehe 24 Septemba 2021, katika kesi hiyo ndogo iliyotokana na pingamizi la utetezi dhisi ya maelezo ya onyo ya mshtakiwa huyo, wakitaka hasitumike kama ushahidi wa jamhuri, ukidai yalichukuliwa kinyume cha sheria.

Mbali na Mbowe na Kasekwa wengine; ni Halfan Bwire Hassan na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!