August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kipa wa Yanga atua Polisi Tanzania

Metacha Mnata

Spread the love

 

ALIYEKUWA golikipa namba moja wa mabingwa wa kihistoria Yanga ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Metacha Mnata amesajiliwa na maafande wa Polisi Tanzania. Anaripoti Wiston Josia, TUDARCo … (endelea).

Metacha ambaye ni kipa wa Taifa Stars, amejiunga na Polisi Tanzania yenye maskani yake Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Usajili wake umekuwa wa kimyakimya kwani tangu alipoachana na Yanga, haikufahamika haraka atakwenda wapi hadi.

Si Metacha mwenyewe au timu yake mpya iliyoweka wazi usajili wake hadi tarehe 11 Septemba 2021, Polisi Tanzania ilipotoa orodha ya wachezaji itakaowatumia kwenye msimu wa 2021/22 kuonesha uwepo wa jina lake.

Yeye mwenyewe Mnata, jana Jumapili tarehe 26 Septemba 2021, ameweka picha kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram akiwa amevalia uzi wa maafande hao wa Polisi Tanzania.

Kikosi cha Polisi Tanzania

Metacha ambaye aliachana na Yanga baada ya kutokea kutokuelewana na kumfanya kusimamishwa kwa miezi kadhaa, amekwenda kukutana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Yanga, Kelvin Yondani.

Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza kesho Jumatatu, Polisi Tanzania itashuka ndimbani kwa mara ya kwanza keshokutwa Jumanne, kuwakabili vijana wa Kinondoni (KMC), katika Uwanja wa Ushirika Moshi.

Kivutio kwenye mechi hiyo ni makipa wa timu zote huenda akawa Metacha Mnata na upande wa KMC, Farouk Shikalo ambaye naye alikuwa Yanga.

Metacha na Shikalo ambaye ni raia wa Kenya wote kwa pamoja walikuwa Yanga na wameondoka wakati mmoja kwa kila mmoja kutafuta fursa kwingine.

error: Content is protected !!