Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Wanaosema huyu mama hamna kitu, nitaongea nao kwa kalamu
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Wanaosema huyu mama hamna kitu, nitaongea nao kwa kalamu

Spread the love

 

KWA mara ya pili Rais Samia Suluhu Hassan amewakemea watumishi wanaodhani kuwa yeye ni mpole na kurudia kusisitiza kuwa ataongea nao kwa kalamu. Anaripoti Patricia Kighono –TUDARCo … (endelea). 

Pia ameeleza kukerwa na mameya, wenyeviti madiwani na watumishi wa mamlaka za serikali za miitaa ambao wanagombana, hawashirikiani wala kuheshimiana.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Septemba 2021 wakati akihutubia wajumbe Mkutano Mkuu maalumu wa uchaguzi wa viongozi wakuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT).

“Najua kuna wanaonitizama nilivyo na wakasema huyu mama hamna kitu. Nilisema ndani ya miezi sita nilikuwa nawasoma na ninyi mmenisoma kwa hiyo sasa tumesomana kazi iendelee.”

Amewaambia viongozi hao wanaogombana kwamba wasidhani huko walipo hawaoni.

“Mkurugenzi anasema hili mwingine anasema lile, DC anasema hili DAS wake anasema lile, kuna mivutano na sioni sababu kwanini mvutane, watu mmeamininiwa, mmeteuliwa na mmpelekwa huko kutumikia wananchi. Miongozi kanuni sheria zipo sioni kwanini mnavutana.”

Aidha, amesema sababu ya mvutano huo ni fedha zinapoingia ambapo kila mtu anataka amege fungu lake kwanza atie mfuko kabla ya kwenda kwenye maendeleo ya wananchi lakini pili ni pale mwingine anaposimama kwenye sheria mivutano inaanza.

“Nilisema kwenye mkutano niliyowaapisha mawaziri niliyowabadilisha kuwa sitakaa kwenye viriri kufoka sijaumbwa, sijakuzwa hivyo, mimi yangu kuangalia performance zenu, ambaye ipo chini namwambia waziri sijaridhika na huyu namtoa, watu ni wengine mno wanasubiri hizo nafasi, naweka wengine watakwenda kujituma na kutumikia wananchi.

“Msitegemee nitakuiteni fulani na fulani njooni hapa, kwa nini hivi na hivi! Hapana… wote watu wazima mnayajua mazuri na mabaya, mkifanya mnafanya makusudi nitaongea kwa kalamu narudia tena,” amesema Rais Samia.

1 Comment

  • Asante rais ssh kwa kauli yako ya busara na imara sasa wanakuelewa na wasaidizi wako wanatimiza wao wachache bado hawajakuelewa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!