Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali kujenga bandari ya uvuvi Bagamoyo
Habari za Siasa

Serikali kujenga bandari ya uvuvi Bagamoyo

Spread the love

SERIKALI ina mpango wa kujenga bandari ya uvuvi wilayani Bagamoyo, ili kuimarisha shughuli za uchumi wa buluu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo ameyasema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 19 Septemba 2023, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Bandari ya uvuvi unaogharimu Sh. 266 bilioni na ugawaji boti za kisasa kwa wavuvi, Kilwa Masoko mkoani Lindi.

Amesema bandari hiyo itajengwa pale uchumi wa nchi utakaporuhusu, huku akiweka wazi mpango wa Serikali yake ya kuanzisha maeneo ya ufugaji samaki katika ukanda wa pwani ya bahari.

“Kutokana na ukubwa wa ukanda wa Pwani, tunafikiria pia bandari hii niliyoiona na maboto yanavyoletwa na mradi huu, tunataka kuanzisha maeneo ya ufugaji samaki na bandari hii inaweza ikatosha upande huu. Sababu ukanda wetu wa bandari ni mkubwa tunafikiria kujenga bandari nyingine ya uvuvi pale Bagamoyo hali ya uchumi ikituruhusu,” amesema Rais Samia.

Akizungumzia ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa, Rais Samia amesema ukikamilika utasaidia kutoa ajira zaidi ya 20,000 na kutoa fursa mbalimbali ikiwemo za biashara kwa wananchi wa eneo hilo.

Kuhusu boti za kisasa zilizogawiwa kwa wavuvi, Rais Samia amewataka kurejesha kwa wakati mikopo hiyoili nyingine zinunuliwe kwa ajili ya kuwanufaisha wavuvi wengine.

Aidha, Rais Samia amewataka vijana kuchangia fursa za uvuvi ikiwemo kufuga samaki kwa kuwa masoko ya uhakika yapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!